Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ukoo wa Patel Wachangia Fedha Kwa Ajili ya Upasuaji wa Moyo Kwa Watoto 10 Wanaotibiwa JKCI
Dec 17, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_25140" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Ukoo wa Patel, Harish Patel akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mfano wa hundi ya shilingi 22,500,000/= fedha zitatumika kwaajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.[/caption]

Na: Mwandishi Wetu

Ukoo wa Patel umekabidhi kiasi cha shilingi 22,500,000/= fedha ambazo zitatumika  kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Akikabidhi fedha hizo leo Mwenyekiti wa Ukoo huo Harish Patel alisema watoto wengi wanazaliwa na ugonjwa wa moyo na wengi wao hawana fedha za kulipia matibabu wameona kwa kidogo walichokipata kisaidie kulipa gharama za matibabu ya wagonjwa hao.

[caption id="attachment_25141" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na ukoo wa Patel pamoja na wafanyakazi wa Taasisi hiyo mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi 22,500,000/= fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.[/caption] [caption id="attachment_25142" align="aligncenter" width="750"] Ukoo wa Patel ukiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi 22,500,000/= kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKI) Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.[/caption] [caption id="attachment_25143" align="aligncenter" width="750"] Mkurugezi Mtendaji wa Taasisis ya Moyo Jakaya Kikwete (JKI) Prof. Mohamed Janabi akongea na waandishi wa Habari mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi shilingi 22,500,000/= na Ukoo wa Patel , fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa Moyo kwa watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. (Picha na JKCI)[/caption]

“Kila wakati, kila mwaka kutokana  na kipato tunachokipata tumekuwa tukisaidia jamii katika mambo mbalimbali ikiwemo  elimu na afya na leo hii tumeona furaha zaidi kusaidia watoto”,  alisema.

Akipokea fedha hizo Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI  Prof. Mohamed Janabi aliushukuru Ukoo wa Patel kwa kuona umuhimu wa afya ya mtoto na kusaidia kulipia gharama za matibabu na kuziomba Taasisi, Mashirika na watu binafsi wenye uwezo wajitokeza  kulipia matibabu ya watoto.

Prof. Janabi alimalizia kwa kusema kuwa  watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo ni wengi   kati ya watoto milioni mbili wanaozaliwa asilimia moja (1%) wanazaliwa na matatizo ya Moyo hivyo bado fedha zaidi zinahitajika kwa ajili ya matibabu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi