Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ujenzi Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) Dar -Moro wafikia asilimia 73
Feb 26, 2020
Na Msemaji Mkuu

*Kipande cha Moro-Singida ujenzi wapamba moto*

Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Dar es Salaam mpaka Moro- goro chenye urefu wa kilometa 205 umekamilika kwa zaidi ya asilimia 73 huku utandikaji wa reli ukiwa umemalizika na kazi inayoendelea kwa sasa ni uwekaji wa nguzo za umeme, nyaya pamoja na ujenzi wa vituo mbalimbali vya kuhudu- mia abiria na mizigo.

Akizungumza na Maafisa kutoka Idara ya Habari – MAELEZO, waliofanya ziara

katika mradi huo, Meneja Msaidizi wa mradi wa SGR kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro, Mhandisi Ayouba Mdachi alisema kuwa baada ya ukamilikaji wa utandikaji reli, sasa vituo vinaendelea kujengwa ambapo hadi sasa tayari jumla ya vituo sita kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro viko hatua za mwisho kukami- lika. Aidha katika hatua nyingine kipengele cha pili cha ujenzi huu ni kutoka mkoa wa Morogoro hadi Makutupora Singida ambacho kimekamilika kwa zaidi ya asi- milia 26.

Kwa upande wake Meneja wa Ujenzi wa mradi wa SGR kipande cha Morogoro hadi Singida Makutupora, Mhandisi Faustine Kataraiya alisema “ujenzi huu una- fanyika usiku na mchana na tayari mahandaki manne yamejengwa sehemu mbalimbali zenye milima ambapo treni itapita na madaraja sehemu zenye mito”. Aidha, kati ya mahandaki manne yaliyojengwa Morogoro na Singida, handaki lenye urefu kuliko yote linajengwa chini ya safu za milima ya Ukaguru ambalo lina urefu wa kilometa 1.2, huku daraja kubwa likijengwa mto Mkondoa Moro- goro ikiwa ni utatuzi wa kero ya mafuriko ambayo hupelekea kusimama kwa shughuli za usafiri wa treni kwa kipindi cha msimu wa mvua nyingi kwa reli ya zamani.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi