Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ujenzi Kinyerezi II Wafikia Asilimia 84
Nov 21, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_23144" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (aliyekaa) akipata maelezo kuhusu uzalishaji wa Umeme katika kituo cha Kinyerezi I jijini Dar es Salaam. Waliomzunguka ni watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).[/caption]

Na Teresia Mhagama

Ujenzi wa mitambo ya kuzalisha Umeme wa kiasi cha megawati 240 kwa kutumia Gesi Asilia katika mradi wa Kinyerezi II umefikia asilimia 84.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Meneja Miradi ya Umeme ya Kinyerezi, Mhandisi Stephen Manda wakati akitoa taarifa ya miradi ya Kinyerezi I (MW 150), Kinyerezi I-Extension (MW 185) na Kinyerezi II (MW 240) kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.

Naibu Waziri Mgalu alifanya ziara katika mitambo hiyo lengo likiwa ni kupata taarifa na kukagua kazi iliyofanywa na Wataalam wa TANESCO ya kusafisha na kuunga Bomba kubwa la Gesi katika mitambo ya Kinyerezi I iliyofanyika Novemba 18 na 19 mwaka huu na hivyo kusababisha upungufu wa Umeme katika Gridi ya Taifa.

  [caption id="attachment_23145" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akikagua mitambo ya uzalishaji wa Umeme katika kituo cha Kinyerezi I jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja Mitambo ya Kinyerezi I, Ernest Nzemya na kushoto kwake ni Meneja Miradi ya Umeme ya Kinyerezi, Mhandisi Stephen Manda.[/caption]

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli hiyo, Mhandisi Manda alieleza kuwa TANESCO walikamilisha zoezi hilo kwa ufanisi na ilipofika mchana wa Novemba 20, 2017 mitambo hiyo iliingiza megawati 115 katika Gridi ya Taifa na hivyo kuboresha hali ya upatikanaji wa Umeme.

Kuhusu mradi wa Kinyerezi II unaotekelezwa na  Mkandarasi SUMITOMO    kutoka   nchini Japan, Mhandisi Manda alisema kuwa matarajio ni kuanza kuzalisha Umeme mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka huu ambapo megawati 30 zitaanza kuingizwa katika Gridi ya Taifa.

Aidha, alisema kuwa matarajio ni mitambo hiyo kuongeza megawati 30 kwenye Gridi ya Taifa kila mwezi mpaka zitakapokamilika megawati 240 mwezi Julai, 2018.

Alieleza kuwa, Mkandarasi wa mradi huo anatarajia kukabidhi mradi husika kwa Serikali Septemba 30, mwaka 2018 na kuongeza kuwa

[caption id="attachment_23146" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Mitambo ya Kinyerezi I inayozalisha Umeme wa kiasi cha megawati 150 I jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_23147" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa Nne kushoto) akipata maelezo kuhusu kazi iliyofanyika na wataalam wa TANESCO ya kusafisha na kuunga Bomba kubwa la Gesi katika mitambo ya Kinyerezi I iliyofanyika Novemba 18 na 19 mwaka huu. Anayetoa maelezo ni Meneja Miradi ya Umeme ya Kinyerezi, Mhandisi Stephen Manda (wa tatu kushoto).[/caption]  

Wataalam wazawa watakaoendesha kituo hicho tayari wamepata mafunzo kutoka nje na ndani ya nchi.

Kuhusu utekelezaji wa mradi wa Kinyerezi I-Extension (MW 185), alisema kuwa utekelezaji wake umefikia asilimia 48 na kwamba ujenzi wa misingi yote ya mitambo na viambata vyake imekamilika.

Aliongeza kuwa, mitambo yote ya Umeme itakayotumika kwenye mradi huo imeshatengenezwa na ipo tayari kuletwa nchini baada ya kukaguliwa na wataalam na kwamba Wataalam wa TANESCO wapo nchini Norway kwa ajili ya kukagua mifumo ya uendeshaji wa mitambo hiyo kabla kusafirishwa kuja nchini.

kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati aliwapongeza wataalam wa TANESCO kwa kusimamia kwa umakini miradi hiyo na kuwataka kuendelea kufanya kazi usiku na mchana ili kuweza kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.

       

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi