Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Ugawaji Vitambulisho vya Taifa Waanza Mkoani Dodoma
May 08, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Mwandishi Wetu

Zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu mkoani Dodoma linaendelea sambamba na ugawaji Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi ambao wamekamilisha hatua zote za usajili.

Akielezea mafanikio hayo Afisa Usajili wa Wilaya ya Dodoma, Khalid Mrisho amesema Wilaya yake imejipanga katika kuhakikisha kukamilika kwa usajili kunakwenda sambamba na kasi ya Uzalishaji ili kuwawezesha wananchi kupata vitambulisho vyao kwa wakati badala ya kusubiri kwa muda mrefu.

“Ugawaji wa vitambulisho kwa sasa umerahisishwa tofauti na zamani ambapo mtu ilikuwa lazima kufika ofisi zetu kuchukua Kitambulisho lakini kwa sasa kutokana na usajili unaoendelea kwenye mitaa na vijiji vitambulisho vikishazalishwa wananchi wanapelekewa huko huko walipo kupitia watendaji wa Mitaa na Vijiji wanakoishi kuwagawia kama inavyoendelea sasa kwenye baadhi ya mitaa” alisisitiza.

Amesema ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa unaofanyika sasa kwenye ofisi ya Wilaya ni kwa wale watumishi wa Umma tu ambao kwa sababu mbalimbali walishindwa kufika kuchukua Vitambulisho vyao sambamba na kufanya usajili kwa watumishi wapya ambao hapo awalli hawakusajiliwa lakini kwa wananchi vitambulisho wanachukulia kwenye mitaa na vijiji waliko.

Sambamba na zoezi la usajili na ugawaji Vitambulisho linaloendelea mkoani humo Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza maandalizi ya zoezi la Usajili wa Machinga maarufu kama Watarazaki, zoezi linalolenga kuwapatia vitambulisho vitakavyowawezesha kufanya shughuli zao za kibiashara bila kubughudhiwa.

Baadhi ya mikoa tayari wameanza usajili wa Wamachinga maarufu Watarazaki ambao zoezi hilo linalenga kuwapata vitambulisho vya biashara ambavyo utambuzi wake unategemea Utambulisho wa Taifa.

Kwasasa Ugawaji Vitambulisho vya Taifa unafanyika katika Ofisi za Watendaji wa Mitaa na kwenye Ofisi ya Wilaya ya Dodoma iliyoko ghorofa namba 5 Jengo la Hazina.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi