Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Uchumi wa Tanzania Watarajiwa Kuendelea Kukua
Jun 17, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_53250" align="aligncenter" width="750"] Akizungumza leo Jijini Dodoma, wakati wa shughuli za kuvunja Bunge la kumi na moja, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Maguful[/caption]

Na Jacquiline Mrisho, Dodoma

Kutokana na hatua zilizochukuliwa na nchi ya Tanzania katika kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na Virusi vya Corona, uchumi wake unatarajiwa kuendelea kuwa na matokeo chanya katika ukuaji wake.

Kauli hiyo imetolewa jana Bungeni, jijini Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wakati akilivunja Bunge la 11 ambapo alimshukuru Mungu kwa kuivusha Tanzania katika janga hilo.

Rais Dkt. Magufuli amefafanua kuwa maamuzi yaliyochukuliwa kukabiliana na ugonjwa huo yamejidhihirisha kuwa sahihi kwani mpaka sasa, kwa kiasi kikubwa, sio tu kufanikiwa kuushinda ugonjwa huo lakini pia kupunguza athari zake, zikiwemo athari za kiuchumi.

“Kama mnavyofahamu, Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), yamebashiri kwamba asilimia 60 ya nchi za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara zitashuhudia ukuaji hasi wa uchumi mwaka huu wa 2020. Hata hivyo, sisi Tanzania, kutokana na hatua tulizochukua, uchumi wetu unatarajiwa kuendelea kukua vizuri kwa asilimia 5.5”, alisema Rais Magufuli.

Amebainisha mafanikio mengine yakiwemo ya kulinda ajira za wananchi wa Tanzania, kuwa na uhakika wa usalama wa chakula na pia kuendelea na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati.

Aidha, amewapongeza wabunge kwani pamoja na hofu kubwa iliyokuwa imetawala, Bunge hilo liliendelea na vikao vyake kama kawaida kwa lengo la kuwatumikia Watanzania.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi