[caption id="attachment_35006" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kuimarisha sekta ya nishati hapa nchini, ili kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda, wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini leo Jijini Dodoma.[/caption]
Na: Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja Umetajwa Kusaidia Upatikanaji wa Nishati hiyo Kuwa wa uhakika na kuzuia kupanda kwa Bei Kiholela Katika Kipindi cha Miaka 2 iliyopita na hivyo Kuchochea Maendeleo hapa nchini.
Akizungumza wakati wa Semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa Serikali imefanikiwa kuhakikisha kuwa upatikanaji wa mafuta hapa nchini ni wa uhakika ikilinganishwa na kipindi cha kabla ya kuanza kwa utaratibu wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja.
[caption id="attachment_35007" align="aligncenter" width="750"]“ Dhamira ya Serikali ni kuendelea kuhakikisha kuwa, kupitia uagizaji wa mafuta wa pamoja upatikanaji wa mafuta hapa nchini unaendelea kuwa wa uhakika, unaoendana na mahitaji ya Taifa Letu,” Alisisitiza Dkt. Kalemani.
Akifafanua Dkt. Kalemani amesema kuwa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja unatekeleza majukumu yake kwa ufanisi hali iliyopelekea kutokuwepo kwa changamoto za mafuta yasiyo na ubora, kukosekana kwa mafuta na kupanda kwa bei mara kwa mara hali iliyokuwa ikijitokeza kabla ya mwaka 2015.
“Kwa sasa tumepanua wigo wa uingizaji mafuta hapa nchini kwa kuongeza Bandari za Tanga na Mtwara ambazo tayari zimeanza kupokea shehena ya mafuta hivyo kupunguza umbali kutoka mafuta yanapopokelewa hadi kwa watumiaji wa nishati hiyo” Alisisitiza Dkt. Kalemani
[caption id="attachment_35009" align="aligncenter" width="900"]Akizungumzia faida za utaratibu wa uagizaji mafuta kwa pamoja Dkt. Kalemani amesema kuwa ni pamoja na; Serikali kusimamia kwa ukaribu sekta ya nishati, upatikanaji wa kodi stahiki kulingana na kiwango kilichoingizwa nchini, kuepusha vitendo vyovyote vya kuhujumu sekta hiyo muhimu kwa maendeleo na ustawi wa wananchi.
Aliongeza kuwa kwa sasa, kwa mwezi Wakala wa Uagizaji wa mafuta kwa pamoja unaingiza lita elfu 98 za Petroli, Dizeli zaidi ya 147,000, mafuta ya Taa lita 6000 na ya ndege 12,000.
[caption id="attachment_35011" align="aligncenter" width="900"]Akizungumzia mafuta yanayopitishwa hapa nchini kuelekea nchi jirani Dkt. Kalemani amesema kuwa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja unaratibu vizuri mafuta yote yanayopitishwa kwenda nchi jirani kwa kuhakikisha kuwa taratibu zote zinafuatwa kwa mujibu wa sheria Kanuni na taratibu.
Semina kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imefanyika kwa wajumbe hao leo Jijini Dodoma ikishirikisha Wenyeviti wa Bodi za Mashirika yaliyopo chini ya Wizara ya Nishati ikiwemo EWURA na TPDC.