Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tuzo ya Kiswahili ya Heshima ya Shaaban Robert Kuanza Kutolewa Mwakani
Jun 22, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33071" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akipokelewa na Mkuu wa Idara ya Kiswahili wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John (SJUT), Bi. Lilian Kaishozia alipowasili chuoni hapo kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Kiswahili, "Mtazamo Mpya" kilichoandikwa na mwanazuoni mkongwe na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiswahili Development Ltd (KIDE -MAKI), Profesa David Masamba (hayupo pichani) Jijini Dodoma. Katikati Kampuni ya Kiswahili Development Ltd (KIDE -MAKI), Athuman Sungura na Mkurugenzi wa Uendeshajio na Masoko, Majid Mswahili. Uzinduzi huo umeambatana na kongamano la Kumbukizi ya mwanafasihi nguli Hayati Shaban Robert.[/caption]

Na: Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Tuzo ya Kiswahili ya Heshima ya Shaaban Robert inategemea kuanza kutolewa mwaka 2019 na Kampuni ya Maendeleo ya Kiswahili (KIDE - MAKI) kwa watu mbalimbali wanaoendelea kuienzi na kuikuza lugha ya Kiswahili.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amethibitisha hayo leo kwenye uzinduzi wa kumbukizi ya Shaaban Robert na Tamasha la Ustaarabu wa Mswahili uliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Chuo cha Mt. John jijini Dodoma.

[caption id="attachment_33072" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Kiswahili kilichoandikwa na mwanazuoni mkongwe na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiswahili Development Ltd (KIDE -MAKI), Profesa David Masamba (kushoto) leo katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John(SJUT) Jijini Dodoma. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Boniphace Kadili. Uzinduzi huo umeambatana na kongamano la Kumbukizi ya mwanafasihi nguli Hayati Shaban Robert.[/caption] [caption id="attachment_33073" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiswahili Development Ltd (KIDE -MAKI), Profesa David Masamba akisoma taarifa fupi kuhusu Kampuni hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Kiswahili alichokiandika mwenyewe leo katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John(SJUT) Jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. Uzinduzi huo umeambatana na kongamano la Kumbukizi ya mwanafasihi Hayati Shaban Robert.[/caption]

Dkt. Mwakyembe amesema kuwa tuzo hizo zitatolewa katika tamasha Kubwa la ‘Ustaarabu wa Mswahili’ litakalokuwa likifanyika kwa siku tatu za mwezi Januari kila mwaka.

“Tuzo hizo zitatolewa katika kilele cha tamasha hilo ambapo watu na taasisi mbalimbali zilizojipambanua kipekee katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili zitatunukiwa”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Dkt. Mwakyembe ameongeza kuwa Serikali inaunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau wa lugha ikiwemo Kampuni hiyo katika mambo yanayolenga kukuza, kueneza na kuendeleza lugha nchini.

  [caption id="attachment_33074" align="aligncenter" width="1000"] Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John (SJUT) anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Yohana Petro Msanjila akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Kiswahili kilichoandikwa na mwanazuoni mkongwe na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiswahili Development Ltd (KIDE -MAKI), Prof. David Masamba(wapili kutoka kushoto) leo katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John(SJUT) Jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Boniphace Kadili na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. Uzinduzi huo umeambatana na kongamano la Kumbukizi ya mwanafasihi nguli Hayati Shaban Robert.[/caption] [caption id="attachment_33076" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akishiriki kuimba wimbo wa Taifa alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Kiswahili, "Mtazamo Mpya" kilichoandikwa na mwanazuoni mkongwe na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiswahili Development Ltd (KIDE -MAKI), Profesa David Masamba (kushoto) leo katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John(SJUT) Jijini Dodoma. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Boniphace Kadili. Uzinduzi huo umeambatana na kongamano la Kumbukizi ya mwanafasihi nguli Hayati Shaban Robert.[/caption]

Pia amefafanua kuwa juhudi hizo ni moja ya utekelezaji wa sera hivyo kinachotakiwa sasa ni ubidhaishaji wa lugha ya Kiswahili ili kiendelee kuleta manufaa na kuongeza tija kwa wananchi.

Akiongelea kuhusu Kumbukizi ya Hayati Shaaban Suleimani Juma Ufukwe (Shaaban Robert), Dkt. Mwakyembe amesema kuwa juhudi zake zimechangia sana kukua kwa lugha ya Kiswahili ambapo kwa hivi sasa ni lugha ya 10 kati ya lugha 6000 zinazozungumzwa duniani.

“Chemchem za mawazo yake, tifutifu za mielekeo yake, mboji za maarifa na mafunzo ya nguli na jabali wa Fasihi ya Kiswahili bado yanatuongoza vema hata leo katika maono ya nchi yetu ya kuwa na uchumi wa kati kupitia Tanzania ya viwanda”, alisema Dkt. Mwakyembe.

[caption id="attachment_33077" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akionyesha Kitabu cha Historia ya Kiswahili, "Mtazamo Mpya" kilichoandikwa na mwanazuoni mkongwe na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiswahili Development Ltd (KIDE -MAKI), Profesa David Masamba (kushoto) katika hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John(SJUT) leo Jijini Dodoma. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Boniphace Kadili. Uzinduzi huo umeambatana na kongamano la Kumbukizi ya mwanafasihi nguli Hayati Shaban Robert.[/caption] [caption id="attachment_33079" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kulia), Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John (SJUT) anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Yohana Petro Msanjila (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Boniphace Kadili wakiwa wameshikilia Kitabu cha Historia ya Kiswahili, "Mtazamo Mpya" katika hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John(SJUT) leo Jijini Dodoma. Kitabu hicho kimeandikwa na Profesa Masamba ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiswahili Development Ltd (KIDE - MAKI).[/caption] [caption id="attachment_33080" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akimkabidhi zawadi ya kitabu cha Historia ya Kiswahili, "Mtazamo Mpya" mmoja wa wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John(SJUT) leo Jijini Dodoma. Kitabu hicho kimeandikwa mwanazuoni mkongwe na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiswahili Development Ltd (KIDE -MAKI), Profesa David Masamba (kushoto), uzinduzi huo umeambatana na kongamano la Kumbukizi ya mwanafasihi nguli Hayati Shaban Robert.[/caption] [caption id="attachment_33081" align="aligncenter" width="768"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari Kikuyu zilizopo Jijini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Kiswahili, "Mtazamo Mpya" kilichoandikwa na mwanazuoni mkongwe na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiswahili Development Ltd (KIDE -MAKI), Profesa David Masamba (mwenye suti nyeusi kulia)uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John(SJUT) leo Jijini Dodoma. Uzinduzi huo umeambatana na kongamano la Kumbukizi ya mwanafasihi nguli Hayati Shaban Robert. (Picha na: Frank Shija - MAELEZO, Dodoma)[/caption]

Aidha katika kumbukizi hiyo, Waziri Mwakyembe amezindua kitabu cha “Historia ya Kiswahili kwa Mtazamo Mpya” kilichotungwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo ambaye amebobea katika uandishi wa vitabu vya kifasihi, Prof. David Massamba.

Kitabu hicho kinatoa ufafanuzi wa kina kuhusu historia na asili/chimbuko la lugha ya Kiswahili na Waswahili na kuziba mapengo ya kuwepo kwa mkanganyiko au ukinzani wa wanazuoni mbalimbali kuhusu historia na asili  ya lugha ya Kiswahili na Mswahili ambao umedumu kwa muda mrefu sana.

Shaaban Robert alikuwa ni mwandishi nguli wa vitabu vyenye maudhui mbalimbali vikiwemo vya Kusadikika, Kufikirika pamoja na Adili na Nduguze, alizaliwa Januari Mosi, 1909 na kufariki June 22,1962.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi