[caption id="attachment_42702" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora Mhe. Gift Msuya akisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia hati milki za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo wakati akifungua mafunzo kwa wakulima zaidi ya mia moja wa Kijiji cha Miyenze Wilayani humo baada ya kurasmisha mashamba yao na kupatiwa hati za hakimiliki za kimila, Mpango wa urasimishaji unatekelezwa na Ofisi ya Rais- MKURABITA.[/caption]
NA TIGANYA VICENT
WAKAZI wa Kijiji cha Miyenze wilayani Uyui wametakiwa kutumia hati za hakimiliki za kimila walizopewas kuomba mikopo itakayowawezesha kuboresha kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati wa kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wa Kijiji cha Miyenze na kukabidhi hati za hakimiliki ya ardhi za kimila kwa wakazi 100.
Alisema wakazi walipata hati za haki miliki hizo za kimila wanao usalama wa zao za ardhi na wameiongezea thamani ambayo inawafanya kuwa na fursa za kupata fedha.
Msuya aliongeza kuwa hati hizo zitawasaidia kupata dhamana hata kwenye vyombo vya kisheria kama vile Mahakama pindi wanatakiwa kuweka mali isiyo hamishika.
Alisema hati walizopata ni fursa pia ya kuwawezesha kuingia ubia na wawekezaji mbalimbali ambao wanatafuta ardhi inayotambulika kisheria kwa ajili ya kuwekeza katika sekta za viwanda, hoteli, maduka na shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wakazi wa Kijiji hicho na maeneo mengine katika wilaya hiyo ambao mashamba yao hayajapimwa kuhakikisha wanaypima ili kuyaongezea thamani na kuwaondoa katika umaskini na kupunguza migogoro.
Alisema hakuna haja ya wananchi kukumbatia maeneo makubwa ambayo hayajapimwa kwa kuwa hayawezi kuwasaidia kupata maendeleo yao na nchi kwa ujumla kwa kuwa ni sawa na mali mfu.
[caption id="attachment_42712" align="aligncenter" width="750"]Kwa upande wa Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu alisema kuwa pamoja na kutoa hati hizo watawajengea uwezo wakulima 100 na viongozi 10 jinsi ya kuendesha kilimo bora na utunzaji wa kumbukumbu za hesabu za kilimo na biashara.
Alisema maeneo mengine ni jinsi ya kutafuta fursa na kuzitumia na ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara na uandishiwa mpango wa biashara na uundaji wa vikundi vya uchumi.
Naye mmoja wa wakulima wa Kijiji cha Miyenze William Mauye aliishukuru Serikali kwa kuwawezesha kupima mashamba yao na hatimaye kuwapatia hati za haki miliki za kimila kwa kuwa zitawasaidia kuinua kipato chao kwa kuwa watakuwa na fursa ya kupata mikopo ya benki.
Alisema mkopo atakaochukua utamwezesha kununuza zana za kilimo za kisasa kwa ajili ya kuboresha kilicho chake cha mpunga na mahindi na hivyo kuongeza uzalishaji.
Mauye aliiomba Serikali kupitia MKURABITA kuendelea kuwasaidia wananchi wa vijiji ili wapimie ardhi yao na kuepuka baadhi ya watu ambao wakuwa wakichukua fedha zao bila hata kuwapimia maeneo yao.
[caption id="attachment_42717" align="aligncenter" width="750"]