Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tume ya Utumishi wa Walimu Yatajwa Kuongeza Ubora Sekta ya Elimu
Oct 06, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_17446" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe. Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo alipokutana na ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Walimu ulipotembelea Wilaya hiyo mapema leo ukiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Tume hiyo Bi. Devotha Gabriel.

[/caption] [caption id="attachment_17449" align="aligncenter" width="750"] Katibu Tawala wa Wilaya ya Kongwa Bw. Audiphace Mushi akieleza jinsi uwepo wa Ofisi za Tume ya Utumishi wa Walimu Wilayani humo ilivyoongeza tija katika kutoa huduma kwa walimu wakati ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Walimu ulipotembelea Wilaya hiyo mapema leo.[/caption]

Frank Mvungi- Maelezo – Dodoma

Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) imetajwa kuwa kiungo muhimu katika kuwawezesha walimu kutoa mchango wao utakaosaidia kukuza Kiwango cha elimu hapa nchini.

Akizungumza wakati wa ziara ya Ujumbe wa Tume hiyo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Deogratius Ndejembi amesema kuwa anaipongeza Tume hiyo kwa kuweka mkazo katika matumizi ya TEHAMA.

[caption id="attachment_17452" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu akimuonesha Katibu Msaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Bw. Edward Chamwela namna ya kutumia mfumo rasmi wa barua pepe za Serikali (GMS) ili kuimarisha Mawasiliano ngazi ya Wilaya na Taifa.[/caption]

“Teknolojia ni jambo muhimu sana katika kusaidia kuharakisha maendeleo na kuongeza ufanisi kwa kuondoa udanganyifu unaoweza kujitokeza katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kuwahudumia wananchi “ Alisisitiza Ndejembi

Akifafanua  zaidi Mhe. Ndejembi amesema mifumo ya TEHAMA inayoenda sambamba na mahitaji ya ulimwengu wa sasa ni chachu ya maendeleo hapa nchini.

[caption id="attachment_17455" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe. Deogratius Ndejembi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Tume ya Utumishi wa walimu mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake mapema leo ukiongozwa na Mkuu wa kitengo cha TEHAMA wa Tume hiyo Bi Devotha Gabriel .
[/caption] [caption id="attachment_17458" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe. Deogratius Ndejembi akiagana na Mkuu wa kitengo cha TEHAMA wa Tume ya Utumishi wa Walimu Bi Devotha Gabriel mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake leo Wilayani Kongwa.[/caption]

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Audiphace Mushi amesema kuwa Tume imewezesha walimu kutambua haki na wajibu wao,kusaidia walimu kupata haki zao kwa wakati.

Tume ya utumishi wa Walimu imekuwa mhimili muhimu katika kuwasimamia walimu hivyo ni vyema kila mdau akasaidia juhudi za Tume ili kuimarisha utendaji wake.

Tume ya Utumishi wa Walimu imetembelea Wilaya za Chemba, Bahi, Chamwino,Kondoa, Mpwapwa na Kongwa ili kujionea hali halisi ya utendaji wa Makatibu Wasaidizi wa Tume ngazi ya Wilaya hali itakayochochea na kuhamasisha wadau kujitokeza na Kusaidia Tume kukabiliana na changamoto zinazowakabili walimu kote nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi