[caption id="" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Mhe. Vumilia Nyamoga akisisitiza jambo mapema leo wakati akizungumza na ujumbe kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu ulioongozwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Tume hiyo Bi. Devota Gabriel.[/caption]
Frank Mvungi-Maelezo Dodoma
Tume ya Utumishi wa Walimu nchini imepongezwa kwa utendaji mzuri unaoendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano yakujenga mazingira mazuri kwa walimu na watumishi wa sekta hiyo kote nchini.
Akizungumza Ofisini kwake Leo Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Mhe. Vumilia Nyamoga amesema kuwa Tume hiyo imeonyesha dhamira njema kwa kujenga mifumo ya TEHAMA itakayowaunganisha makatibu wasidizi wa Tume hiyo katika Wilaya zote nchini na makao makuu ya Tume hiyo hali itakayochochea kuongezeka kwa ufanisi.
[caption id="attachment_16598" align="aligncenter" width="1000"]Mhe. Nyamoga amesema kuwa anaridhishwa na jinsi Tume hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika Wilaya hiyo kwani inafanya kazi nzuri na yakupigiwa mfano katika kuwahudumia walimu.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Tume hiyo Bi. Devota Gabriel amesema kuwa dhamira yao ni kuhakikisha kuwa makatibu wasidizi wa Wilaya takribani 139 kote nchini wanaunganishwa katika mifumo ya TEHAMA ukiwemo ule wa barua pepe rasmi za Serikali (GMS) ili kuongeza ufanisi ambapo zoezi hilo limeanza katika baadhi ya Wilaya za Mkoa wa Dodoma ikiwemo Chemba, Chamwino na litahusisha Wilaya zote za Mkoa huo.
[caption id="attachment_16601" align="aligncenter" width="1000"]Aidha Bi. Devota alitoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kushirikiana na Tume hiyo katika kufanya tafiti mbalimbali ili kuongeza tija kwa Taifa na wananchi kwa ujumla kutokana na matokeo ya tafiti hizo.
Kwa upande wake Katibu Msaidizi wa Tume hiyo Wilaya ya Chamwino Bw. Khalid Shaban amesema kuwa pamoja na Tume hiyo kuwa na Umri wa mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake viongozi wake akiwemo Katibu wa Tume hiyo Mwalimu Winifrida Rutaindurwa na Mwenyekiti Ndugu Oliver Mhaiki wameonyesha dhamira ya dhati katika kuwahudumia walimu.
[caption id="attachment_16600" align="aligncenter" width="1000"]“ Viongozi wote wameonyesha njia kwa kufika katika Wilaya zetu na kuangalia changamoto za walimu na kuanza mara moja kutafuta ufumbuzi ili kuchochea ukuaji wa sektaya elimu hapa nchini” alisisitiza Shaban.
Tume ya Utumishi wa Walimu imeanzishwa kwa sheria namba 25 ya mwaka 2015 na imeweza kuanza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.