Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tume ya Uchaguzi Yawaonya Watakaoharibu Uchaguzi
Oct 24, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37282" align="aligncenter" width="800"] Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mbarouk Salum Mbarouk akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wa uchaguzi yanayofanyika jijini Dodoma ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika majimbo manne na kata 47 za Tanzania Bara.[/caption]

Na: Margareth Chambiri -NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewaonya Wasimamizi wa Uchaguzi ambao ama kwa kujua au kwa makusudi wataharibu au kukiuka taratibu za Uchaguzi kutokana na kutofuata sheria na taratibu za Uchaguzi.

Onyo hilo limetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk wakati akifungua mafunzo kwa Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi jijini Dodoma.

[caption id="attachment_37286" align="aligncenter" width="800"] Baadhi ya wakuu wa idara kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na wasimamizi wa uchaguzi kUtoka halmashauri mbalimbali wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi.[/caption]

Mheshimiwa Mbarouk ambaye amewataka Wasimamizi hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea amesema Sheria ya Taifa ya Uchaguzi na ile ya Serikali za Mitaa zinaunda kosa la jinai na kutoa masharti ya adhabu kwa Afisa yeyote wa Uchaguzi ambaye atasababisha kuharibu uchaguzi.

Makamu Mwenyekiti huyo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amesema madhara ya kutozingatiwa kwa taratibu za Uchaguzi ni kusababisha kesi nyingi za Uchaguzi na kuitumbukiza Serikali katika gharama ambazo zingeweza kutumika katika shughuli nyingine za maendeleo.

Amewataka Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kuyaelewa vyema maeneo wanayofanyia kazi na kujiamini ambapo pia amewakumbusha jukumu walilo nalo la kuimarisha imani ya wananchi na wadau wengine wa Uchaguzi kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi wakisaini viapo ikiwa ni utekelezaji wa sharia za uchaguzi. [caption id="attachment_37289" align="aligncenter" width="800"] Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Dodoma Arnold Kirekiano akiwaongoza kiapo kwa wasimamizi wa uchaguzi kabla ya mafunzo ya usiamamizi wa uchaguzi.[/caption] [caption id="attachment_37290" align="aligncenter" width="800"] Mkurugezi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia akifafanua hoja kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia kwa wasimamizi wa uchaguzi.[/caption] [caption id="attachment_37291" align="aligncenter" width="800"] Baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia, wakati akitoa mada kuhusu mambo ya kuzingatia kwa wasimamizi wa uchaguzi.[/caption] [caption id="attachment_37292" align="aligncenter" width="800"] Mkuu wa Idara ya Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Irene Kadushi, akifafanua jambo wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi.[/caption] [caption id="attachment_37294" align="aligncenter" width="800"] Mkuu wa Idara ya Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Emmanuel Kawishe akifafanua hoja katika mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi.[/caption] [caption id="attachment_37295" align="aligncenter" width="800"] Afisa Uchaguzi Meshack Mgovano, akieleza jambo kwenye mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi. (Picha zote na NEC)[/caption]

Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt Athumani Kihamia amewataka washiriki wa mafunzo hayo kutoa ushirikiano kwa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mdogo ikiwa ni pamoja na kuvishirikisha katika kila hatua muhimu wakati wa mchakato wa Uchaguzi.

Dkt. Kihamia amesema Watendaji wote wa Tume wanapaswa kuwapo katika maeneo yao ya kazi wakati wote hususan kipindi cha Uteuzi, kufungua ofisi hadi muda wa kisheria na Vyama vyote ambavyo vimefuata taratibu vipewe fomu za Uteuzi na Wagombea wao wateuliwe kama wamekidhi vigezo.

Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi ameongeza kusema kuwa kutozingatiwa kwa mambo hayo husababisha kuharibu imani ya Wadau na kusababisha malalamiko ya kutoridhishwa na mchakato wa Uchaguzi na hatimaye mashauri ya Uchaguzi kufikishwa mahakamani.

Kadhalika Dkt Kihamia amewataka Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi hao wa Uchaguzi kutojihusisha na migogoro ya ndani ya Vyama na iwapo Vyama vitakuwa na malalamiko vielekezwe kuwasilisha malalamiko yao kwenye Kamati za Maadili na si mahali pengine popote.

Kwa mujibu wa Dkt. Kihamia chaguzi zote duniani ni kielelezo cha demokrasia na kwamba Uchaguzi huru na wa haki hutokana na Wasimamizi wa Uchaguzi wanaozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia Uchaguzi husika.

Jumla ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi 210 kutoka katika Majimbo manne ya Serengeti, Simanjiro, Ukerewe na Babati Mjini pamoja na Kata 47 zinazotarajiwa kufanya Uchaguzi Mdogo Desemba 3, mwaka huu wanashiriki katika mafunzo hayo yatakayodumu kwa siku tatu jijini Dodoma.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi