Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Trilioni 3 .7 Kujenga Barabara za Lami, Kuondoa Changamoto ya Uchukuzi na Usafirishaji Maeneo ya Vijijini
Aug 27, 2023
Trilioni 3 .7 Kujenga Barabara za Lami, Kuondoa Changamoto ya Uchukuzi na Usafirishaji Maeneo ya Vijijini
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali akizungumza Agosti 26 ,2023 jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa Serikali.
Na Mwandishi Wetu

Shilingi Trilioni 3.7 kutumika katika ujenzi wa barabara za lami  zenye urefu wa kilomita 2,035 .

Ujenzi wa barabara hizo umebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Agosti 26 ,2023 jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.

" Wakandarasi wa kutekeleza miradi hii tayari wamepatikana  na mikataba ya ujenzi wake imeshasainiwa ili kazi iendelee", alisisitiza Msigwa.

Akitaja miradi hiyo Msigwa amesema wa kwanza ni ule wa  Kidatu , Ifakara, Lupiro Malinyi , Kilosa, Mpepo, Londo, Lumecha hadi Songea wenye urefu wa kilomita 512.

Mradi mwingine ni ule wa  Arusha, Kibaya  hadi Kongwa wenye urefu wa Kilomita 493.

Msigwa aliongeza kuwa mradi mwingine ni wa Handeni, Kibereshi, Kijingu, Njoro, Olboroti, Mrijo chini, Dalai, Bicha, Chambolo, Chemba, Kwa Mtoro Singida wenye urefu wa Kilomita 460.

Miradi mingine ni pamoja na ule wa Igawa, Songwe hadi Tunduma wenye urefu wa kilomita 218.

Pia, mradi wa Masasi Nachingwea wenye urefu wa Kilomita 81.

Mradi wa mwisho kwa mujibu wa Msigwa ni ule wa Karatu, Mbulu, Hydom, Sibiti, Lalago hadi Maswa mkoani Shinyanga wenye urefu wa Kilomita 389.

Serikali ya Awamu ya Sita imeweka mkazo katikati ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja, viwanja vya ndege na mingine kwa lengo la kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi jumuishi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi