Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TBS Yatumia SHIMMUTA Kutoa Elimu Kanda ya Ziwa
Dec 08, 2019
Na Msemaji Mkuu

Na Mwandishi wetu,

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ni moja ya washiriki kwenye mashindano ya SHIMMUTA yaliofanyika Mkoani Mwanza kwa taktibani siku 15 ambayo yalihusisha taasisi, makampuni na mashirika arobaini na sita (46) kutoa mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Afisa Masoko Mwandamizi wa TBS, Bi, Gladness Kaseka alisema, wametumia fursa ya kushiriki mashindano hayo kutoa elimu kuhusu umuhimu wa viwango kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya kijamii.

Bi. Kaseka alisema kuwa TBS imetoa elimu juu ya taratibu za kufuata ili kusajili bidhaa na majengo, taratibu za kupata leseni ya kutumia alama ya ubora, shughuli zinazofanywa na kituo cha teknolojia cha vifungashio, shughuli za uandaaji viwango hususani viwango vya madini, umuhimu wa kuzingatia ubora/usalama katika chakula na vipodozi na njia mbalimbali wanazotumia kutoa elimu ya viwango kwa umma.

Bi. Kaseka alifafanua kwa kusema kuwa elimu hiyo iliyotolewa kupitia Radio Kwizera, Radio Free Afrika,Radio Metro, Star Tv na mitandao mbalimbali ya kijamii imelenga kumfungua mtumiaji na mzalishaji wa bidhaa kujua umuhimu wa viwango katika maisha yake kwani kazi ya kupiga vita bidhaa hafifu ni ya kila mmoja katika jamii, na ilienda sambamba na kuwakumbusha wananchi kutumia dawati la huduma kwa wateja ambalo linatoa fursa kwa watu wote kutoa maoni, malalamiko na maulizo masaa 24 kupitia barua pepe ya _malalamiko@tbs.go.tz au simu ya bure 0800110827.

TBS imefanya vizuri kwenye mashindano hayo haswa katika mchezo wa mpira wa miguu na kuvuta kamba, ambapo mpira wa miguu waliingia robo fainali na kuvuta kamba nusu fainali huku ikiibuka mshindi wa tatu katika mchezo wa kuvuta kamba baada yakuwavuta mzobemzobe TANESCO.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi