Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TBS Yatoa Elimu kwa Wananchi 14000 Kanda ya Ziwa
Feb 18, 2019
Na Msemaji Mkuu

Na Neema Mtemvu - TBS

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limemaliza Kampeni yake ya kutoa Elimu kwa umma katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa na shirika hilo.

Kampeni hiyo ya Elimu kwa umma imefanyika katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Shule za Msingi na Sekondari, Masoko, Stendi, Minadani na maeneo mengine ya wazi ambapo wananchi walijitokeza kupata elimu na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo Ubora wa Bidhaa.

Kwa upande wake Afisa Masoko Mwandamizi, Bi.Gladness Kaseka amewakumbusha Wananchi wote kuwa vita ya bidhaa hafifu sio ya TBS pekee bali ni ya Taifa kwa ujumla.

"Kampeni hii imeweza kuwafikia wananchi 14, 929 kati yao wajasiriamali 127,wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari 3868 na wananchi 10,934," Alisema Kaseka.

Aliwasisitiza wananchi kuendelea kutoa taarifa kupitia mawasiliano waliyopewa pale wanapogundua uwepo wa bidhaa hafifu katika soko.

Vilevile Shirika lilipata fursa ya kutoa semina kwa wajasiriamali wanaojihusisha na bidhaa mbalimbali zikiwemo za nafaka, sabuni, maziwa, asali na unga lishe juu ya utaratibu wa kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS.

Wajasiriamali hao wadogo walitolewa hofu kuwa huduma hiyo inatolewa bure.

Kampeni hiyo imefanyika katika Wilaya za Bukoba, Kahama, Tarime na Nyamagana.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi