Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TBS Yakamata Vipodozi Hatarishi kwa Matumizi ya Binadamu
Nov 23, 2019
Na Msemaji Mkuu

Shirika la Viwango Tanzania limekamata vipodozi vyenye viambata sumu katika ukaguzi uliofanyika Mkoani Singida.Ukaguzi huo umefanyika Mkoani hapo kuanzia Novemba 11, mwaka huu na Maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na linatarajiwa kuhitimishwa Novemba 25, mwaka huu.

Ukaguzi  huo wa kushtukiza uliofanyika  kwenye maduka ya kuuza vipodozi na kufanikiwa kukamata vipodozi vyenye viambata sumu, ambavyo vimepigwa marufuku kutokana na kuwa na madhara kwa binadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari Manyoni leo Mkaguzi wa Shirika hilo, Domisiano Rutahala alisema   kwamba zoezi hilo limefanyika Singida maeneo ya Singida Manispaa, Kiomboi , Shelui,Mkalama,itigi na Manyoni

 "Tumefanikiwa kukamata vipodozi vyenye viambata sumu ambavyo vimepigwa marufuku kutokana na kuwa na madhara kwa watumiaji.Vipodozi hivyo vinaondolewa kwenye soko kutokana na kuwa na madhara mbalimbali kwa watumiaji. Alisema Rutahala

Aliongezea pia Baadhi ya madhara  ya vipodozi hivyo ni kusababisha saratani ya ngozi, kupunguza kinga ya ngozi na kuathiri mfumo wa homoni za mwili.

 Rutahala, aliwashauri watumiaji kuacha kutumia vipodozi vilivyopigwa marufuku na kutoa wito kwa wafanyabiashara kuacha kuviuza.

Wakati huo huo, shirika la Viwango limewataka wenye maduka ya chakula na vipodozi kujisajili kupitia mfumo unaopatikana kwenye tovuti ya shirika hilo, ili waweze kupatiwa vibali vinavyotakiwa kwa ajili ya kufanya biashara hizo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi