Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TAYARH Yaanzisha Kampeni dhidi ya ukatili wa Kijinsia.
Nov 01, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_21520" align="aligncenter" width="750"] Mratibu wa Taasisi inayojihusisha na masuala ya utetezi wa haki za kundi la balehe na vijana (TAYARH) Bw. Lameck Laurence (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mitandaoni ya kuwapatia vijana elimu juu ya uzazi wa mpango na huduma bora za afya leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwanachama wa taasisi hiyo Godlove Isdory, kushoto ni mratibu wa mradi huo mtandaoni Godfrey Mitande.[/caption]

Na: Thobias Robert- Maelezo

Taasisi inayojihusisha na masuala ya utetezi wa haki za kundi balehe na vijana nchini (TAYARH) imezindua kampeni ya mtandaoni (Online campign) yenye lengo la kuwezesha vijana kupata taarifa sahihi na huduma bora juu ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango.

Kampeni hiyo imezindilwa leo Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa taasisi hiyo Lameck Laurence alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya kampeni hiyo itakayofanyika kwa muda wa wiki nne ambayo pia itakuwa kampeni mwendelezo kwa Tanzania bara na Visiwani.

“Tumelenga kuwafikia vijana takribani laki 2 kwa njia ya mtandao katika kipindi cha wiki nne za kampeni yetu. Tutakuwa na mijadala kila siku kupitia kurasa za Facebook, Instagram na Twitter, hivyo vijana wengi watapata taarifa sahihi kuhusu uzazi wa mpango na afya ya uzazi. Tutatumia Hashtag #Jiongeze katika kipindi chote cha kampeni,” alieleza Laurence.

[caption id="attachment_21521" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wananchama wa Taasisi inayojihusisha na masuala ya utetezi wa haki za kundi la balehe na vijana (TAYARH) wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mitandaoni ya kuwapatia vijana elimu juu ya uzazi wa mpango na huduma bora za afya uliofanywa na taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.[/caption]

Aidha aliongeza kuwa TAYARH itatumia njia ya radio pamoja na televisheni kuwafikia watanzania wengi hususani wasio na uwezo wa kutumia simu za kisasa (Smartphone).

Aliendelea kusema kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na chama cha waandishi wa habari wanawake (TAMWA) na Ofisi ya Taifa ya takwimu (NBS) zinaonesha kuwa kati ya mwaka 2012 na 2013 matukio yapatayo 228 ya mimba na matukio 42 ya ndoa za utotoni yaliripotiwa Tanzania.

“Visiwani Zanzibar, hali ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ilionekana zaidi katika maeneo ya mkoa wa Kusini Pemba na Wilaya ya Kati Unguja. Kwa upande wa Tanzania bara ukatili ulionekana zaidi katika Wilaya za Kahama, Sengerema, Tarime, Newala, Mbulu, Bunda, Nkasi, Babati, Chunya, Dodoma, Bariadi, Busega, na Singida vijijini,” alifafanua Laurence.

Aliendelea kusema kuwa, kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita asilimia 17 ya wanawake wamefanyiwa vitendo vya ukatili vinavyohusisha ngono, ambapo asilimia 9 kati yao wamepata unyanyasaji wa kijinsia unaohusisha vitendo vya ngono.

Mratibu huyo alifafanua kuwa, vitendo vya ukatili unaohusiana na ngono vimekuwa vikiongezeka sambamba na umri kuanzia asilimia 8 kwa wanawake wenye umri wa miaka 15-49 hadi asilimia 18 kwa wanawake wa umri miaka 40-49.

Kuhusu suala la uzazi wa mpango mratibu huyo alisema kuwa, asilimia 62 ya wanawake wenye umri wa miaka kati ya 15-49 wanaotumia njia za kisasa za mpango waliambiwa kuhusu madhara ya njia hizo ambapo asilimia 56 walielezwa nini cha kufanya endapo madhara yangewakuta. Aidha aliongeza kuwa asilimia 82 ndio walielezwa kuhusu kupatikana kwa njia zingine za uzazi wa mpango.

“Tunaamini kuwa kampeni hii itasaidia kutokomeza changamoto mbalimbali zinazowakumba vijana katika masuala ya uzazi wa mpango na elimu ya afya ya uzazi, itawasiaidia wanajamii kutambua umuhimu wa kuapata huduma bora za afya ya na matumizi sahihi ya njia za uzazi wa mpango ili kutokomeza umaskini, mimba za utotoni na unyanyasaji wa kijinsia hapa nchini,” alisisitiza Bw.Laurence.

TAYARH ni muunganiko wa taasisi zinazojihusisha na masuala ya utetezi wa haki za kundi balehe na vijana Tanzania. Muunganiko huo ulianza mwaka 2016 na kutiwa saini ya kufanya kazi kwa pamoja mwaka 2017. Taasisi hii imeundwa na asasi za Tanzania Youth Vision Association, Youth of United Nations Associations, YAM-UMATI, African Young Adolescent Network, Zanzibar Fighting Against Youth Challenge Organization, Restless Development, pamoja na International Youth Alliance on Family Planning.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi