Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tatizo la Maji Lindi Mjini Kubaki Historia
Feb 01, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_28366" align="aligncenter" width="800"] Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo akisikiliza maelezo kutoka kwa mshauri muelekezi wa mradi maji wa Ng'apa Mkoani Lindi bw.Colman Ngainayo (wakwanza kulia), wakati wa ziara yake yakukagua mradi huo wenye thamani ya Euro milioni 11.7 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali, mradi huo utawanufaisha wakazi wa Lindi mjini kuanzia leo Februari mosi, kushoto ni meneja wa mradi huo kutoka Kampuni ya OIA ya nchini india Bw. Rajeev Rai.[/caption] [caption id="attachment_28367" align="aligncenter" width="804"] Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la mradi wa maji wa Ng'apa Mkoani Lindi utakaowanufaisha wakazi wa Lindi mjini kuanzia leo Februari mosi.[/caption]

Na Mwandishi Wetu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo amefanya ziara kutembelea mradi wa maji wa Ng'apa Mkoani Lindi wenye thamani ya Euro milioni 11.7 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali.

Profesa Mkumbo amesema kuwa wananchi wa Lindi wanaanza kupata huduma ya maji leo Februari mosi huku kazi ndogondogo zilizobaki katika mradi huo zikiendelea kukamilishwa.

Akifafanua amesema kuwa mradi huu unatarajia kuzalisha kiasi cha lita milioni 7 za maji kwa siku kiasi ambacho kitakidhi mahitaji ya maji Lindi mjini kwa sasa na kuchochea ukuaji wa uchumi na uzalishaji, Aidha mahitaji ya maji ya mji huo ni kiasi cha lita milioni 5 kwa siku .

“ Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Lindi (LUWASA) itafanya kazi ya ukarabati wa miundombinu iliyopo pamoja na kuongeza mtandao katika vitongoji ambavyo havina mtandao wa mabomba “ Alisisitiza Profesa Mkumbo.

Aidha, Profesa Mkumbo ametoa wito kwa wananchi Mkoani Lindi kulinda miundombinu ya maji na kulipa ankara za maji waliyotumia ili huduma hiyo iwe endelevu na ichangie katika kuleta maendeleo.

Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeweka mkazo katika kuimarisha huduma za jamii hasa zile zinazowagusa wananchi wanyonge ikiwemo upatikanaji wa maji safi na Salama kwa wananchi wake kote nchini hali inayochochea kasi yautekelezaji wa miradi ya maji katika Mikoa na Wilaya mbalimbali hapa nchini.

Mradi huo umetekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji ambapo mkandarasi ni Kampuni ya OIA ya nchini india.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi