Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TASAC Yatoa Elimu ya Ulinzi, Usalama na Utunzaji wa Mazingira Morogoro
Nov 14, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Mwandishi Wetu,Morogoro

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imetoa elimu ya usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira mkoani Morogoro pamoja na kuendesha zoezi la ukaguzi wa Vyombo vya usafiri majini.


Ukaguzi huo ni sehemu ya mikakati ya Shirika hilo kuhakikisha vyombo vya usafiri majini vinakuwa na ubora unaotakiwa kwa kuzingatia viwango. 


Zoezi hilo liliendeshwa na Maafisa Ukaguzi na Udhibiti wa Vyombo vya Majini  wa Shirika hilo, Bw. Gabriel Manase na Maulid Nsalamba katika Wilaya ya Ifakara mkoani humo. Maafisa hao walitoa elimu ya usalama na ulinzi ikiwemo utunzaji wa mazingira wanapokuwa kwenye shughuli zao.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Manase alisema elimu hiyo ina umuhimu mkubwa sana hivyo jamii inapaswa kuitambua na kuweza kuzingatia wakati wote wanapotekeleza shughuli zao za kila siku.

Zoezi hili lilianza tarehe 11 Novemba, 2022 Ifakara katika maeneo ya Ngalimila, Ngapemba, Utengule, Chita na Mngeta na Mchombe na litaendelea katika Mikoa ya  Iringa na Dodoma lengo ni kuhakikisha jamii inapata elimu.

Zoezi hilo liliendeshwa pia kwa ushirikiano na Afisa Masoko Mwandamizi wa TASAC, Martha Kelvin na Afisa Uhusiano Mwandamizi, Amina Miruko ambapo waliitaka jamii kuhakikisha inazingatia usalama kwenye vyombo vya maji ili kuweza kuepukana na ajali ambazo zinazaweza kuwakuta wawapo safarini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi