Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TARURA Kujenga Kilomita 427 za Lami
Aug 24, 2023
TARURA  Kujenga  Kilomita 427 za Lami
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji na mipango ya Wakala kwa mwaka 2023/2024.
Na Na Mwandishi Wetu

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa mwaka wa fedha 2023/2024, imejipanga kujenga jumla ya barabara zenye KM 427 kwa kiwango cha lami, KM 21,057.06 kufanyiwa matengenezo, KM 8,7775.62 kujengwa kwa kiwango cha changarawe, kujenga madaraja na makalavati 855 pamoja na mifereji ya mvua KM 70.

Hayo yameelezwa leo Agosti 24, 2024 jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Mhandisi Victor Seff wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji na mipango ya Wakala kwa mwaka 2023/2024.

“Jumla ya shilingi bilioni 858.517 zimeidhinishwa kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara za wilaya, kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 710.31 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 148.207 ni fedha za nje kupitia miradi ya RISE, TACTIC, Bonde la mto Msimbazi na Mradi wa Agri connect”, amebainisha Mhandisi Seff.

Aidha, akizungumza kuhusu matumizi ya teknolojia mbadala na malighafi zinazopatikana maeneo inapotekelezwa miradi  ya ujenzi wa barabara na madaraja, Mhandisi Seff anasema kuwa, “ Moja ya kipaumbele cha TARURA ni kutumia malighafi zinazopatikana maeneo husika ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi.”

Ameongeza kuwa, hadi mwezi Machi, 2023 TARURA imejenga madaraja 163 ya mawe yenye thamani ya shilingi bilioni 8.7 ambapo gharama imepungua kwa zaidi ya asilimia  50, madaraja hayo yamejengwa katika mikoa ya Kigoma 92, Singida 24, Tabora 5, Kilimanjaro 10, Mbeya 2, Arusha 6, Morogoro 2, Rukwa 3, Pwani 1, Ruvuma 3 na Iringa 15.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inasimamia ujenzi, ukarabati na matengenezo ya mtandao wa barabara za wilaya, aidha tafiti zinaonesha kuwa maeneo ya kilimo vijijini yakiwa yanafikiwa kwa mwaka mzima, inaongeza ukuaji wa kilimo  na kupunguza umaskini  ambapo takribani asilimia 65.1 ya Watanzania wanaishi vijijini na sekta ya kilimo kwa Tanzania inachangia Pato la Taifa kwa takribani asilimia 26.

Umuhimu wa barabara za vijijini  unaisukuma Serikali kuhakikisha kuwa zinapitika misimu yote ya mwaka  ili kuchangia ukuaji wa kilimo na kupunguza umaskini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi