Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania - Zambia Wajadili Masuala ya Ushirikiano
Oct 11, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zambia zinakutana jijini Lusaka, Zambia kujadili masuala ya ushirikiano yaliyokubaliwa baina ya nchi hizo mbili.

Majadiliano hayo yanafanyika katika Mkutano wa Kumi wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano - ngazi ya wataalam unaofanyika leo tarehe 11 Oktoba, 2022.

Mkutano huu utafuatiwa na mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 12 Oktoba, 2022 na mwisho utamalizika kwa mkutano ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 14 Oktoba, 2022 jijini Lusaka Zambia.

Mkutano huu unajadili na kutathimini utekelezaji wa maazimio katika sekta mbalimbali za ushirikiano zilizokubaliwa katika mkutano wa tisa uliofanyika tarehe 25 hadi 26 Februari, 2016 jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Maeneo ya ushirikiano ni pamoja na; Siasa, Ulinzi na Usalama, Mambo ya Nje, Uhamiaji, Fedha na Uchumi, Sheria, Nishati, Habari na Mawasiliano, Kilimo, maendeleo ya miundombinu, Uchukuzi na Usafirishaji, Elimu, Sayansi na Teknolojia, Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Utalii, Kilimo, Uvuvi, Mazingira na Maliaasili, Afya, Elimu, Vijana na Michezo na jinsia.

Mkutano huu unafanyika kufuatia maagizo ya Marais wa pande zote mbili wakati wa ziara ya kiserikali ya Rais wa Jamhuri ya Zambia nchini Tanzania, Mhe. Hakainde Hichilema mapema mwezi Agosti, 2022.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi