Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania Yatekeleza kwa Kasi Mradi wa Bomba la Mafuta
May 02, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_31097" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt. Medard Kalemani (wa Tatu kulia), Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Irene Muloni (katikati), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, (wa Tatu kushoto), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt Adelardus Kilangi (wa Pili kushoto) na Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira, Kazi na Vijana, Anthony Mavunde (kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam kutoka Tanzania na Uganda mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika jijini Kampala.[/caption]

Imeelezwa kuwa, Tanzania inatekeleza kwa kasi masuala mbalimbali yatakayopelekea mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanzania kuanza kutekelezwa ndani ya muda uliopangwa.

Hayo yamebainika hivi karibuni wakati wa kikao kati ya Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt. Medard Kalemani na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Irene Muloni jijini Kampala nchini Uganda kilicholenga kupata taarifa na kujadili Maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.

Katika kikao hicho, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani aliambatana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  Dkt Adelardus Kilangi na Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira, Kazi na Vijana, Anthony Mavunde.

[caption id="attachment_31094" align="aligncenter" width="1000"] Mawaziri mbalimbali kutoka Tanzania na Uganda pamoja na Watendaji mbalimbali kutoka nchi hizo wakiwa katika kikao na wawekezaji wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanzania kilichofanyika jijini Kampala hivi karibuni.[/caption]

Kutokana na kasi hiyo ya Wataalam wa Tanzania, Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda aliwaasa Watalaam wa Uganda kufanya bidii ili kwenda na kasi ya utekelezaji wa mradi huo ili ukamilike mapema mwaka 2020 kama ilivyopangwa.

Vikao vya Mawaziri vilitanguliwa na vikao vya Wataalam na Makatibu wakuu kutoka Tanzania na Uganda ambapo  katika vikao hivyo Mawaziri wa nchi husika pamoja na wawekezaji katika mradi huo walijadili masuala  mbalimbali zikiwemo changamoto za utekelezaji wa mradi ili kuweza kuzitatua.

Vilevile, Viongozi na Wataalam walijadili masuala  ya Kisheria na Biashara yanayotakiwa kutekelezwa kwa pamoja.

[caption id="attachment_31095" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Irene Muloni wakijadiliana jambo mara baada ya kufanya kikao kilichojadili masuala mbalimbali kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka nchini Uganda hadi Tanzania.[/caption]

Katika vikao hivyo, Timu ya Watalaam ya Uendelezaji wa Mradi wa Bomba iliongozwa na Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Petroli, Mwanamani Kidaya ambaye pia alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati katika Vikao vya Makatibu Wakuu.

Wawekezaji katika mradi huo ni Kampuni za Total E&P ya Ufaransa, Tullow Oil ya Uingereza, China National Offshore Oil Company (CNOOC) na kampuni za Mafuta za Taifa za Tanzania na Uganda.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi