Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania Yaendelea Kurekodi Kasi Ndogo ya Kupanda Kwa Mfumuko wa Bei Afrika Mashariki
Oct 08, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na; Frank  Mvungi

Mfumuko wa Bei kwa mwezi Septemba, 2018 umefikia asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.3 kwa mwaka unaoishia mwezi Agosti, 2018 ambapo Tanzania imeendelea kuwa na  kiwango kizuri cha mfumuko wa bei ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Akizungumza leo Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo amesema kuwa pamoja na ongezeko hilo dogo Tanzania bado inafanya vizuri ambapo kiwango chake cha kasi ya kupanda kwa bei kiko chini ukilinganisha na nchi zingine za Afrika Mashariki.

Akieleza sababu za ongezeko hilo dogo la mfumuko wa bei, bwana Kwesigabo amesema chanzo chake ni kupanda bei kwa bidhaa zisizo za vyakula. Baadhi ya bidhaa hizo ni pamoja na vinywaji baridi, vileo na bidhaa za tumbaku, vifaa vya matengenezo na ukarabati wa nyumba n.k.

Mfumuko wa bei nchini ni asilimia 3.4 wakati nchi ya Kenya ina asilimia 5.70 kutoka 4.04 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2018. Nchi ya Uganda imerekodi punguzo la mfumuko wa bei kutoka asilimia 3.8 hadi asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia Agosti 2018.

Akifafanua zaidi amesema kuwa mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwezi Septemba, 2018 umeendelea kupungua hadi asilimia 2.0 kutoka asilimia 2.2 ilivyokuwa mwezi Agosti, 2018.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi