Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania Miss Super Model Akabidhiwa Bendera Kuliwakilisha Taifa Mashindano ya Dunia
May 19, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_1307" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi akizungumza wakati wa tukio la kumkabidhi bendera ya Taifa mshiriki wa mashindano ya Miss Word Super Model 2017, Miss. Asha Ally Mabula (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam. Miss huyo anatarjia kuondoka leo kuelekea Macau nchini China ambapo atashiriki mashindano hayo.[/caption]

Na Nuru Juma & Husna Saidi

Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah kihimbi amemkabithi bendera ya Taifa Tanzania Miss Super Model 2017 Asha Ally Mabula kwa ajili ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia ya  Miss Super Model yanayotarajia kufanyika 21hadi 28 mei katika mji wa Macau nchini China. Akimkabidhi bendera hiyo, Bi Leah alisema kuwa ana amini Miss huyo ataenda kuliwakilisha vyema Taifa la Tanzania katika mashindano hayo ya Dunia ambapo alimuhakikishia kuwa  Wizara pamoja na Watanzania  wapo pamoja nae kwa kipindi chote ambacho atakuwa huko. “Mrembo wetu anatakiwa kukumbuka kuwa katika mashindano hayo anaenda kuliwakilisha Taifa hivyo Watanzania tunamsihi asiende kufanya vitu vitakavyoiharibu sifa ya nchi yetu  na badala yake aende kuishi kwa mila na desturi zetu za kitanzania ,” alisema  Leah. [caption id="attachment_1308" align="aligncenter" width="750"] Miss Super Model 2017 Asha Ally Mabula akizungumza wakati wa tukio la kukabidhiwa bendera ya Taifa kwa ajili ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Miss Word Super Model 2017 leo Jijini Dar es Salaam. Miss huyo anatarajia kuondoka leo kuelekea Macau nchini China ambapo atashiriki mashindano hayo. Kutoka kulia ni Afisa Utumishi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bi. Flora Mgonja, Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi na Meneja Mkuu wa Tanzania Miss Super Model Ibrahim Thabit.[/caption] Aidha alimsisitiza kufanya vizuri katika kuwania taji hilo lakini pia  kulitangaza Taifa na kuweza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania na  kutangaza utalii na utamaduni wa nchi hasa katika matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili. Naye Tanzania Miss Super Model Asha Mabula ameishukuru Serikali kwa kuweza kumkabidhi bendera hiyo ya Taifa na  ameahidi kwenda kuitangaza Tanzania katika masuala ya utalii, kulinda heshima yake na Taifa kwa ujumla  na kushiriki vyema ili kuhakikisha anarudi na Taji la Miss World Super Model. Hata hivyo Asha aliwaomba Watanzania kushirikiana nae katika maombi na kuwa nae bega kwa bega kwa kila hatua atakayoifanya ili kumpa moyo  kwani anaenda kule kuiwakilisha Tanzania na si yeye kama Asha. Mshindi huyo wa Tanzania Miss Super Model anatarajiwa kuondoka nchini  leo kwenda Macau China kwa ajili ya kushiriki mashindano  ya Miss World Super Modal yanayotarajia kufanyika kuanza Mei 21 hadi 28 mwaka huu. [caption id="attachment_1312" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi akimkabidhi bendera ya Taifa mshiriki wa mashindano ya Miss Word Super Model 2017, Miss. Asha Ally Mabula (kushoto) wakati wa hafla ya kumkabidhi bendera hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. Miss huyo anatarajia kuondoka nchini leo kuelekea Macau nchini China ambapo atashiriki mashindano hayo. Katikati ni Afisa Utumishi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bibi. Flora Mgonja.[/caption] [caption id="attachment_1313" align="aligncenter" width="750"] Baahi ya waandishi wa habari wakishuhudia tukio la kumkabidhi bendera ya Taifa mshiriki wa Miss Word Super Model, Asha Ally Mabula anayetarajia kushiriki mashindano hayo Macau nchini China. (Picha na: Frank Shija)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi