Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania, Marekani Kushirikiana Ufadhili wa Michezo
Oct 03, 2023
Tanzania, Marekani Kushirikiana Ufadhili wa Michezo
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akipeana mkono na Balozi wa Marekani hapa nchini, Mhe. Michael Battle mara baada ya mazungumzo yao waliyoyafanya leo Oktoba 3, 2023 jijini Dar es Salaam.
Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amefanya mazungumzo na Balozi  wa Marekani hapa nchini, Mhe. Michael Battle yaliyojikita katika kuendeleza Sekta za Wizara hiyo.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Oktoba 3, 2023 jijini Dar es Salaam, Mhe. Dkt. Ndumbaro amemueleza Balozi huyo nia ya Tanzania kuwasilisha mapendekezo ya matumizi ya lugha ya Kiswahili katika Umoja wa Mataifa na kuomba nchi hiyo iunge mkono suala hilo, kwa kuwa lugha hiyo tayari inatumika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika na Umoja wa Afrika.

Kwa upande wake Balozi wa Marekani Mhe. Battle ameipongeza Tanzania kwa kufuzu kucheza Mashindano ya Kombe la Mataifa Barani Afrika yatakayofanyika mwakani nchini Ivory Coast, ambapo amesema nchi yake ipo tayari kutoa ufadhili kwa vijana wenye vipaji katika michezo na Sanaa kwa kuwa Taifa hilo limepiga hatua kwenye eneo hilo, na pia kutoa utalaam kwa makocha wa michezo mbalimbali.

Awali Katibu Mkuu Bw. Gerson Msigwa amesema Tanzania inakusudia kuwa na vituo vya michezo katika majiji pamoja na vituo vya kuhifadhi utamaduni, hivyo ameikaribisha nchi hiyo kuunga mkono jitihada hizo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi