Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tamasha la Wanawake Wajasiriamali kufanyika Mwezi Oktoba Jijini Dar es Salaam
Sep 26, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_15659" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la 11 la Wanawake Wajasiriamali (MOWE) Bi.Anna Matinde akieleza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa tamasha na semina kubwa ya 11 itakayofanyika kuanzia tarehe 24-30 Oktoba, 2017 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake huo Bi.Zubeda Lous.[/caption]

Na:Neema Mathias

Umoja wa wanawake wajasiriamali (MOWE) wameandaa tamasha  la 11 kwa wajasiriamali litakalofanyika kuanzia tarehe 24-30 oktoba , 2017 katika viwanja wa mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam lengo ikiwa ni kupanua wigo wa masoko pamoja na kuonyesha bidhaa na fursa mbalimbali za kijasiriamali zinazopatikana hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam,  Mwenyekiti wa kamati ya tamasha hilo, Bi. Zubeda Kiluwa amesema kuwa, tamasha hilo litakuwa na kauli mbiu isemayo‘Mwanamke mjasiriamali funguka shiriki kujenga Tanzania ya viwanda’

“Tunawaalika wanawake wote popote walipo kushiriki maadhimisho na maonyesho haya kwani yatawahusiha wadau mbalimbali wa maendeleo ya wanawake, Wizara pamoja na taasisi za serikali na mashirika binafsi,”alisema Kiluwa.

[caption id="attachment_15660" align="aligncenter" width="750"] Mjumbe wa Umoja wa Wanawake Wajasiriamali (MOWE) Bi. Blandina Sembo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa utambulisho wa Tamasha na semina kubwa ya 11 itakayofanyika kuanzia tarehe 24-30 oktoba ,2017 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Umoja huo Bi. Naomi Kamba na kutoka kulia ni mjumbe wa MOWE. (Picha na Paschal Dotto)[/caption]

Tamasha hilo litafunguliwa  na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwaijage ambapo wadau watakaoshiriki  kutoa elimu za kijasiriamali katika tamasha hilo ni pamoja na Wakala wa Usajili Biashara na utoaji  leseni (BRELA), TRA, GSM, SIDO, TBS, TFDA pamoja na wawakilishi kutoka  katika benki mbalimbali   ambao kupitia semina hiyo watatoa elimu juu ya ujasiriamali.

Aidha Bi.kiluwa ameleza kuwa gharama zitakazotozwa kwa wajasiriamali watakaoshiriki katika maadhimisho hayo ni shillingi 50,000 kila mmoja, na kwa yeyote atakayeshiriki kwaajili ya uzinduzi, ununuzi na kujionea bidhaa mbalimbali hawatatozwa gharama yoyote.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya tamasha hilo Bi.Anna Matinde amaesema kuwa tamasha hilo halitawahusisha wajasiriamali peke yake bali litawahusisha watu wote lengo likiwa ni kubadilishana mawazo ya kimaendeleo katika kuunga mkono sera ya Tanzania ya viwanda.

“Tanzania itajengwa na watu wengi, kupitiwa mawazo ya wajasiriamali na wale wasio wajasiriamali watapata kujua mambo mbalimbali juu ya elimu ya ujasiriamali, namna ya kujiajiri na kuondokana na wimbi la ukosefu wa ajira,” alifafanua Bi. Matinde.

Aidha Bi. Matinde amefafanua kuwa tamasha hilo halitowahusisha  wanawake pekeyake bali hata wanaume wenye fursa mbalimbali za ujasiriamali wanakaribishwa  kutangaza kazi zao na kujipatia elimu itakayotolewa .

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi