Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Takwimu  Zatajwa Kuchochea Maendeleo  Endelevu
May 24, 2018
Na Msemaji Mkuu

Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira kutoka Ofisi  ya Taifa ya  Takwimu (NBS) Bibi Ruth Minja akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashairia vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala, amani na usalama leo Jijjini Dodoma.

Mtaalamu kutoka Taasisi ya Africa Regional Manager, Global  Partnership for Sustainable Development   Data Bw. Davis Adieno akiwasilisha mada katika Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashairia vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala, amani na usalama leo Jijjini Dodoma ikiratibiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshighulikia Usawa  wa Kijinsia wa Wanawake (UN Women) Bibi  Usu  Mallya akizungumzia maana ya  takwimu za kijinsia wakati wa Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashiria vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala, amani na usalama leo Jijjini Dodoma.

 

Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira kutoka Ofisi  ya Taifa ya  Takwimu (NBS) Bibi Ruth Minja akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi hiyo Bw. Said  Ameir wakati  wa wa Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashiria vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala,  amani na usalama leo Jijjini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wa warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashiria vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya maendeleo endelevu usawa wa kijinsia, utawala,  amani na usalama leo Jijjini Dodoma.

Mratibu wa Mpango Kabambe wa kuboresha na kuimarisha  Takwimu Nchini  (Tanzania Statical Master Plan ) Bw. Philemon  Mahimbo  akiwasilisha mada  wakati wa wa Warsha ya wadau kuhusu hali ya upatikanaji wa Takwimu za viashairia vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya Kimataifa ya Maendeleo  Endelevu,  Usawa wa Kijinsia,  Utawala,  Amani na Usalama leo Jijjini Dodoma.

 

Na Mwandishi  wetu

Warsha ya Wadau Kuhusu  hali ya Upatikanaji wa takwimu za Viashiria vya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Malengo ya Kimataifa ya Maendeleo endelevu, usawa wa Kijinsia, Utawala na  Amani .

Akizungumza wakati wa warsha ya siku mbili Leo  Mjini Dodoma Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Kutoka Ofisi  ya Taifa ya Takwimu  (NBS) Bibi Ruth  Minja amesema kuwa  warsha hiyo ni muhimu  na itasaidia  katika kubainisha  maeneo yanayotakiwa kufanyiwa tafiti na kuzalisha takwimu zitakazotumika katika kuchochea maendeleo mara baada ya kubaini maeneo ambayo bado takwimu zake hazijakusanywa.

"  Warsha hii itatusaidia  kuona ni wapi kuna takwimu ambazo hazijafikiwa kweye maeneo mbalimbali ya kisekta ili ziweze kukusanywa na kusaidia katika kuleta maendeleo" Alilisisitiza  Bibi Ruth.

Akifafanua  amesema kuwa jukumu kubwa la Ofisi hiyo ni kukusanya na kuchambua na hatimaye kutoa takwimu rasmi kwa ajili ya matumizi ya sekta mbalimbali ili kuchochea maendeleo .

Kwa upande wake  mmoja wa wawezeshaji katika warsha hiyo Davis  Adieno kutoka nchini Kenya amesema kuwa wanapongeza hatua iliyochukuliwa ya kuwa na warsha hiyo ya wadau kwa kuwa itasaidia takwimu zinazokusanywa zitasaidia wadau katika kupanga mipango ya maendeleo.

Aliongeza kuwa wadau wamekusanyika katika warsha hiyo ili kujifunza na wataweza kushiriki kikamilifu katika kuondoa  umasikini.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Usawa wa Kijinsia wa wanawake ( UN Women) Bibi Usu Mallya amesema kuwa uchambuzi wa Takwimu unasaidia kuonesha upungufu  wa takwimu zinazotakiwa kukusanywa  katika sekta mbalimbali.

Aliendelea kusema kuwa  Takwimu zilizopo zimenyumbulishwa kijinsia na kupitia warsha hiyo washiriki  wataweza kuendeleza takwimu za kijinsia.

Warsha ya ya Wadau Kuhusu  hali ya Upatikanaji wa takwimu za Viashiria vya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Malengo ya Kimataifa ya Maendeleo endelevu, usawa wa Kijinsia, Utawala na  Amani  inafanyika mjini Dodoma kwa siku mbili ikiwashirikisha wadau kutoka sekta ya umma , Binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi