[caption id="attachment_9531" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bw. James Ihunyo (wapili kushoto) akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyokopeshwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wilayani humo. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (katikati) na viongozi waandamizi kutoka wilayani na Benki ya Kilimo.[/caption]
Na: Said Mkabakuri, TADB
Wakulima wa Kilombero wapata mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wa jumla ya shilingi bilioni mbili ili, kuendeleza miradi ya kilimo cha miwa na mpunga.
Akizungumza wakati wa kukagua miradi hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bw Fransis Assenga amesema; “ nimeridhishwa na maendeleo ya miradi hii, ambayo inachochea ari ya Benki katika kutimiza lengo la Serikali la kukopesha wakulima nchini”
[caption id="attachment_9532" align="aligncenter" width="750"]Aidha, Bw Assenga amewasihi wakulima hao kutumia vema mikopo hiyo, ili kujiletea maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. James Ihunyo aliwaasa wakulima hao kurudisha mikopo kwa wakati ili wakulima wengine waweze kupatiwa mikopo hiyo.
[caption id="attachment_9538" align="aligncenter" width="750"]“Lengo la kuwapa mikopo ni ili kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania, hivyo kuchelewesha kulipa mikopo hiyo kwa makusudi ni kurudisha nyuma juhudi hizi,” amesema Ihunyo.
Miradi iliyotembelewa ni Kapolo AMCOS, Skimu ya Umwagiliaji ya Mkula, Umoja wa Wakulima wa Miwa wa Msolwa Ujamaa na Hope ya Kidatu.