Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TADB Yaja Kimkakati Kuzuia Upotevu wa Mahindi Baada ya Kuvuna
Feb 22, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_40762" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara, Bw. Augustino Matutu Chacha akizungumza na wasindikaji na wadau wa zao la mahindi wakati wa uzinduzi wa mradi maalum wenye lengo la kuchagiza wawekezaji hao katika uongezaji wa thamani wa zao hilo. Mkutano huo umefanyika katika Hotel ya Sea Scape jijini Dar es Salaam.[/caption]

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetoa wito kwa wakulima na wasindikaji wa zao la mahindi kuwekeza katika teknolojia za kisasa kwa lengo la kuzuia upotevu wa mahindi baada ya kuvunwa ili kuleta tija katika mnyororo wa thamani wa zao hilo.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara, Bw. Augustino Matutu Chacha wakati akizungumza na wawekezaji katika usindikaji wa zao la mahindi mara baada ya kuzindua mradi maalum wenye lengo la kuchagiza wawekezaji hao katika uongezaji wa thamani wa zao hilo.

“Natoa wito kwa wasindikaji kutumia fursa za mradi huu ili kuongea tija katika shughuli zao,” amesema.

[caption id="attachment_40761" align="aligncenter" width="750"] Msimamizi wa mradi huo, Bi Eunice Mbando akizungumza na wasindikaji na wadau wa zao la mahindi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi maalum wenye lengo la kuchagiza wawekezaji hao katika uongezaji wa thamani wa zao hilo. Mkutano huo umefanyika katika Hotel ya Sea Scape jijini Dar es Salaam.[/caption]

Kwa upande wake Msimamizi wa mradi huo, Bi Eunice Mbando amesema kuwa mfuko huo umelenga kuwajengea uwezo wasindikaji wa ndao kuwa sehemu ya uongezaji wa thamani wa mnyororo wa zao hilo.

“Tunaamini Mradi huu utasaidia kuzuia upotevu wa mahindi hivyo kuleta tija kwa wakulima wa zao hili,” amesema.

Akizungumza kwa niaba ya wasindikaji walioshiriki katika uzinduzi wa Mradi huo, Bw. Savior Chanay kutoka Kampuni ya Real World ya mkoani Ruvuma ameishukuru Serikali kupitia TADB kwa kuja na Mradi huo ambao utaongeza tija katika mnyororo wa thamani wa mahindi.

“Mradi huu utaleta tija katika shughuli zetu za kila siku hivyo kuongeza uwezekano wa kuongeza kipato kwa wakulima wa mahindi,” amesema.

[caption id="attachment_40760" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara, Bw. Augustino Matutu Chacha akiwa katika picha ya pamoja na Msimamizi wa mradi pamoja na wasindikaji wa zao la mahindi wakati wa uzinduzi wa mradi maalum wenye lengo la kuchagiza wawekezaji hao katika uongezaji wa thamani wa zao hilo. Mkutano huo umefanyika katika Hotel ya Sea Scape jijini Dar es Salaam.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi