Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

TADB Yaendelea Kuchagiza Mapinduzi ya Kilimo Katika Skimu ya Umwagiliaji Mombo Tanga
Sep 28, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_35886" align="aligncenter" width="917"] Timu ya Ukaguzi ikiangalia mandhari ya mifereji inayotumia kumwagilia shamba hilo.[/caption]

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, (TADB) imeahidi kunyanyua kipato cha wakulima wadogo wadogo kupitia ushirika wao kwa kuwapatia mikopo ya gharama nafuu ili waweze kumudu gharama za uzalishaji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa kilimo cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji katika Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo iliyopo mkoani Tanga, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema benki yake imejidhatiti kuwasaidia wakulima wadogo wadogo nchini kwa kuwapatia mitaji itayowawezesha kununua zana bora za kilimo ili kuweza kuongeza uzalishaji kama ilivyoanishwa katika Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP 2).

[caption id="attachment_35887" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine akioneshwa mfuko utakaotumika kufungashia mchele unaozalishwa na Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo. Skimu hii imeweshwa kwa mkopo unaotolewa na TADB.[/caption]

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wa skimu hiyo, Katibu wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo, Bwana Sufian Mohamed aliishukuru serikali kupitia Benki ya Maaendeleo ya kilimo kwa kuwapatia mkopo wa gharama nafuu ambao umeweza kuwanufaisha jumla ya wakulima 429 kati yao wanawake wakiwa asilimia 54, mkopo ambao umeboresha miundo mbinu ya skimu hiyo hali iliyowezesha kuongeza uzalishaji kutoka wastani wa tani 1.9 hadi kufikia tani 6 kwa hekta moja.

Skimu hiyo ya Mombo mpaka sasa imenufaika na mkopo wa mbolea, mbegu bora pamoja na trekta, mashine ya kuvunia na sasa Benki ya Kilimo ipo katika hatua ya mwisho ya kuwapatia mashine ya kukobolea mchele ili waweze kuongeza thamani ya zao la mpunga katika skimu hiyo.

[caption id="attachment_35888" align="aligncenter" width="750"] Timu ya Ukaguzi ikiangalia namna uongezaji wa thamani wa zao la mpunga unavyofanyika,[/caption]  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi