Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wanaotumia Mkaa Watakiwa Kutumia Gesi
Aug 01, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_8042" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) January Makamba akielezea jambo kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na matumizi ya nishati ya mkaa alipokutana na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na: Paschal Dotto

Serikali imezitaka Taasisi za umma zinazotumia mkaa na kuni kubadilishiwa matumizi na kutumia gesi katika shughuli zake ili kusaidia katika uhifadhi wa mazingira.

Hayo yamesemwa na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

Waziri Makamba amesema kumekuwa na jitihada mbalimbali katika kutatua tatizo la matumizi ya nishati ya mkaa na kuni, ili kuweka mazingira safi kwa kutunza misitu na kuepusha ukataji wa miti ovyo.

[caption id="attachment_8043" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) January Makamba akielezea jambo kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na matumizi ya nishati ya mkaa alipokutana na waandishi wa habari Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Frank Shija)[/caption] “Kama mnavyofahamu asilimia 90 ya Watanzania wanatumia mkaa na kuni kama nishati ya kupikia na mwanga, hii inasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira kwa sehemu za vijijini ambapo shughuli ya utengenezaji wa nishati hii hufanyika”. alisema Makamba.

Mnamo mwaka 2016 Ofisi ya Makamu wa Rais iliandaa mkutano wa wadau kushauriana, kujadiliana na kutoa mapendekezo juu ya hali hii ya ukataji miti ovyo, mkutano ambao ulihudhuriwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Nishati na Madini, Chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine pamoja na taasisi mbalimbali za Serikali na zisiso za Serikali katika kutafuta mbinu nishati mbadala kwa wananchi.

Katika ripoti ya pili ya mazingira ya mwaka 2014 inaonesha kuwa Jiji la Dar es salaam pekee linatumia wastani wa tani 500,000 ya nishati ya mkaa kila mwaka na mahitaji haya yanaongezeka kila kukicha.

Kwa mujibu wa taarifa ya Taifa ya ufuatiliaji na tathimini ya Rasilimali za misitu nchini, inaonyesha kiasi cha ekari milioni moja au hekta 372,000 zinaharibika kila mwaka  kiasi ambacho ni kiwango kikubwa cha uharibifu wa misitu.

Aidha Waziri Makamaba amefanya mikutano mbalimbali na wasambazaji wa gesi nchini na kuwaasa kuwa chachu kwa taasisi za Serikali zinazotumia mkaa na kuni, kikubwa ni kubadilisha kutoka kutumia mkaa na kuni na kufunga mitambo ya gesi.

Amezitaja  baadhi ya taasisi hizo ambazo mara nyingi zinatumia kuni ili kupata nishati ya kupikia chakula kuwa ni pamoja na Shule mbalimbali nchini, Magereza, Majeshi, Hospitali, na Vyuo mbalimbali.

Waziri Makamba amesema Serikali imefanikiwa kuwashawishi wamiliki wa mitungi ya gesi ya LPG na CNG na wamekubali kufunga mitambo ya gesi katika taasisi hizo ili kupunguza matumizi ya mkaa na kuni.

Mwishoni mwa mwaka huu (2017) Ofisi ya Makamu wa Rais inatarajia kuandaa na kuratibu maonesho makubwa ya teknolojia ya kupunguza matumizi ya mkaa na kuni zinazotekelezwa na wadau mbalimbali nchini, pia kutakuwa na mashindano ya ubunifu katika teknolojia hiyo muhimu kwa mazingira na misitu  nchini.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi