[caption id="attachment_2731" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia wanakikundi cha Bright Focus (hawapo pichani) wakati akifungua kikundi hicho kilichopo chuo cha Uhasibu Singida.[/caption]
Na RS - SINGIDA
Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu nchini zimetakiwa kutoa elimu itakayosaidia wahitimu kutambua fursa mbalimbali katika kukabiliana na changamoto za maisha.
Rai hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi wakati akizindua kikundi cha Bright Focus katika Chuo cha Uhasibu tawi la Singida chenye lengo la kutambua fursa za kuboresha maisha.
“Natambua kuwa kikundi hiki kitasaidia kubuni mawazo yenye tija, fursa, na mwelekeo wa kuboresha uchumi miononi mwenu na kuelekezana namna bora ya matumizi ya rasilimali mlizonazo hususani rasilimali fedha,” alisema Dkt. Nchimbi.
[caption id="attachment_2693" align="aligncenter" width="750"]Dkt. Nchimbi ameongeza kuwa mawazo ya wanakikundi yanapaswa kuendane na malengo ya kikundi hicho kuanzia mwenendo wa maisha, ufaulu na matumizi ya rasilimali yawe yenye muono wa kutengeneza faida na hasa kujifunza namna ya kuhifadhi akiba.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Kikundi hicho, John Gama amesema kuwa kikundi kina malengo mengi ikiwemo kutoa udhamini kwa wanachuo ambao watashindwa kulipa ada kutokana na sababu mbalimbali.
Ameongeza kuwa kikundi kitaanzisha miradi ya maendeleo kama vile kilimo, biashara ya bajaji na pikipiki, ufugaji wa nyuki na kuanzisha makapuni mbalimbali siku za baadaye kwa ajili ya kuongeze kipato kwa wanakikundi.
Vilevile kikundi hicho kina lengo la kutatua changamoto ya ukosefu wa uzoefu hasa linapokuja suala la ajira kwa kuwaajiri wanachuo katika makampuni watakayoanzisha ili waweze kupata ujuzi.
Kikundi cha Bright Focus kina jumla ya wanachama 89 ambao ni wanachuo, walimu na walezi wa Chuo cha Uhasibu Tawi la Singida, ambapo wamempendekeza Dk. Nchimbi kuwa mlezi wa Kikundi hicho.