Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Taarifa kwa Wakandarasi Wanaotekeleza Miradi ya Kusambaza Umeme Vijijini
Jun 16, 2017
Na Msemaji Mkuu

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatambua kuwa baadhi ya wakandarasi wanaotekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini hawajakamilisha miradi kwa mujibu wa MIKATABA waliyosaini na Wakala (REA).

Aidha, kuna baadhi ya wakandarasi wamekamilisha miradi lakini hawajakabidhi rasmi miradi hiyo na vifaa au hawajafanya marekebisho kasoro zilizobainishwa na wasimamizi wa miradi kutoka (TANESCO na REA).

Kwa tangazo hili, Wakala unawataarifu wakandarasi wote ambao hawajakamilisha matakwa hayo ya kimikataba kufanya hivyo mara moja. Wakandarasi watakaoshindwa kutimiza masharti hayo hawataruhusiwa kushiriki katika zabuni zitakazotangazwa na Wakala (REA) baada ya TANGAZO hili na hatua nyingine zitachukuliwa juu yao kwa mujibu wa mikataba hiyo.

 

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu

Wakala wa Nishati Vijijini (REA)

Jengo la Mawasiliano, Ghorofa ya 2

Barabara ya  Sam Nujoma, 14414

S. L.  P 7990

Dar es Salaam, Tanzania

Barua Pepe: info@rea.go.tz Simu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003 Nukushi: +255 22 2412007

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi