UTEUZI WA KAMATI YA KITAIFA YA KUCHUNGUZA UCHAFUZI WA MAZINGIRA KATIKA MTO MARA
-----------------------------------
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameunda Kamati ya Kitaifa yenye wajumbe 11 kuchunguza uchafuzi wa mazingira uliojitokeza hivi karibuni ndani ya Mto Mara baadaya kutembelea eneo hilo.
Kamati hiyo inaundwa na wajumbe wafuatao:
1. Prof. Samwel Manyele - Kutoka Idara ya Uhandisi wa Kemikali na Madini Chuo Kikuu cha Dar es Salaam– Mwenyekiti
2. Dkt. Samuel G. Mafwenga - Mkurugenzi Mkuu – Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) - Katibu
3. Dkt. Kessy F. Kilulya - Mkuu wa Idara ya Kemia – Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Mjumbe
4. Dkt. Charles Kasanzu - Kutoka Idara ya Jiolojia – Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Mjumbe
5. Bw. Daniel Ndio - Mkurugenzi wa udhibiti na usimamizi wa Kemikali – Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) - Mjumbe
6. Bw. Renatus Shinhu - Mkurugenzi wa Bonde – Mamlaka ya Bonde la Maji la Ziwa Victoria - Mjumbe
7. Bi. Baraka Sekadende - Mkurugenzi wa Kituo - Taasisi ya Utafiti wa Samaki (TAFIRI) Mwanza - Mjumbe
8. Dkt. Neduvoto Mollel - Mamlaka ya Afya ya Mimea na Usimamizi wa Viatilifu (TPHPA) - Mjumbe
9. Bi. Asnath Abel Kauya -Kutoka Ofisi ya Rais –Mjumbe
10. Bw. Yusuph Kuwaya - KutokaOfisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara – Mjumbe na
11. Bw. Faraja Ngerageza - Mkurugenzi Msaidizi - Ofisi ya Makamu wa Rais - Mjumbe
Kamati hii imetakiwa kutoa taarifa ya uchunguzi ndani ya siku saba (7) kuanzia leo 12/03/2022 na kuiwasilisha kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ifikapo tarehe 19 Machi, 2022.
Lulu P. Mussa
MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI