Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Taarifa kwa Umma
Nov 01, 2017
Na Msemaji Mkuu

KUWENI WAZALENDO, WAZIRI MKUU AHIMIZA WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waishio Canada wadumishe mshikamano wao na wawe na uzalendo kwa Taifa lao. Ametoa kauli hiyo jana (Jumanne, Oktoba 31, 2017) wakati akizungumza na Watanzania waishio Toronto, Canada. Waziri Mkuu ambaye yuko Canada kwa ziara ya kikazi, alisema kila Mtanzania anapaswa ahubiri utaifa wake. “Wakati wote ringia nchi yako, unapotakiwa kuisemea nchi yako, isemee vizuri kama ambavyo wengine wanasemea vizuri nchi zao licha ya matatizo waliyonayo.” Alisema Serikali inawasisitiza wananchi wake hasa waishio nje ya nchi, wawe wazalendo na washirikiane kuhakikisha wanazitumia fursa za kimaendeleo vizuri kwa ajili ya manufaa ya nchi yao. Awali, Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Nzoka, alitumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania hao wazingatie sheria za nchi wanayoishi. “Wote sisi tunawatambua kama mabalozi katika nafasi zenu hapa Canada. Tunawashauri muwe raia wema, na muishi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi hii na msisahau mlipotoka, kwani hakuna mahali pazuri kama nyumbani,” alisisitiza.  

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMATANO, NOVEMBA MOSI, 2017.

   

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi