Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Taarifa kwa Umma
Oct 19, 2018
Na Msemaji Mkuu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mtangazaji nguli, Marehemu Isaac Gamba aliyefariki jana nchini Ujerumani.

Dkt. Mwakyembe amemuelezea marehemu Isaac kuwa ni  mmoja wa watangazaji mahiri nchini ambaye amekuwa akifanya kazi zake kwa weledi na kujituma katika vyombo mbalimbal vya habarii vikiwemo Redio Free Africa, Redio Uhuru, ITV na Radio One na  baadae Redio Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle) idhaa ya Kiswahili.

Waziri Mwakyembe ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, uongozi wa Redio Deutsche Welle pamoja na wana tasnia nzima ya habari   kwa kuondokewa na mpendwa wao.

Imetolewa na

Shamimu Nyaki

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

19/10/2018

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi