Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Taarifa kwa Umma
May 11, 2018
Na Msemaji Mkuu

Tume ya Madini iliundwa kwa mujibu wa kifungu cha 21 cha Sheria ya Marekebisho Anuwai ya Sheria ya Madini Na. 7 ya Mwaka 2017. Mnamo tarehe 17 Aprili, 2018, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kulingana na Sheria tajwa, aliteua Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Madini. Ili kutekeleza majukumu yake, Tume ilifanya kikao chake cha kwanza tarehe 30 Aprili, 2018 Jijini Dodoma. Pamoja na mambo mengine, Tume iliazimia mambo  yafuatayo:

  1. Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Madini zitakuwa Jijini Dodoma katika Ofisi za Wizara ya Madini;
  2. Kuimarisha usimamizi wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na marekebisho yake ya Mwaka 2017 kwa lengo la kuhakikisha kuwa Serikali inamiliki hisa zisizopungua asilimia 16 ya mtaji wa Kampuni zinazomiliki migodi ya kati (MLs) na mikubwa (SMLs), Wazawa wanashirikishwa ipasavyo katika Miradi ya Madini na kunufaisha jamii katika maeneo ya migodi na Taifa kwa ujumla;

  • Kuwajulisha wamiliki wote wa leseni zote za kuhodhi maeneo (Retention Licences – Jedwali Na. 1) kuwa leseni zao zimefutwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 ikisomwa pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2017 na Kanuni ya 21 ya Kanuni za Madini (Haki Madini), 2018 Tangazo la Serikali Na.1/2018 na kwamba maeneo ya leseni hizo yamerudishwa Serikalini bila hakikisho la kupewa tena;

Jedwali Na. 1: Orodha ya leseni za kuhodhi maeneo zilizofutwa

Namba ya Leseni Jina la Mmiliki Aina ya Madini Tarehe ya kutolewa Tarehe ya kuisha muda Ukubwa (Km2) Mkoa/Wilaya Hali halisi
RL 0001/2009 Kabanga Nickel Company Limited Nickel 02/05/2009 01/05/2019 201.85 Kagera/ Ngara Imefutwa
RL 0006/2009 National Mineral Development Corporation Limited Gold 31/12/2009 30/12/2019 21.27 Shinyanga/ Kahama Imefutwa
RL 0009/2014 Bafex Tanzania Limited Silver, gold & Copper 01/09/2014 31/08/2019 12.58 Mbeya/ Chunya Imefutwa
RL 0010/2014 Bafex Tanzania Limited Silver, gold & Copper 01/09/2014 31/08/2019 12.59 Mbeya/ Chunya Imefutwa
RL 0011/2014 Bafex Tanzania Limited Silver, gold & Copper 01/09/2014 31/08/2019 11.83 Mbeya/ Chunya Imefutwa
RL 0012/2014 Bafex Tanzania Limited Silver, gold & Copper 24/09/2014 23/09/2019 11.27 Mbeya/ Chunya Imefutwa
RL 0014/2014 Mabangu Mining Limited Gold 31/10/2014 30/10/2019 2.94 Geita/Mbogwe Imefutwa
RL 0015/2014 Resolute (Tanzania) Limited Gold 31/10/2014 30/10/2019 0.91 Geita/Mbogwe Imefutwa
RL 0016/2015 Wigu Hill Mining Company Limited Rare Earth Elements 13/02/2015 12/02/2020 15.14 Morogoro Imefutwa
RL 0017/2015 Nachingwea Nickel Limited Nickel 21/04/2015 20/04/2020 48.8 Lindi /Nachingwea Imefutwa
RL 0013/2014 Precious Metals Refinery Company Limited Nickel 10/10/2014 09/10/2019 25.7 Simiyu/ Bariadi & Busega Imefutwa

  1. Hadi kufikia tarehe 04/07/2017, kulikuwa na jumla ya maombi mapya ya leseni za uchimbaji wa kati (MLs) zipatazo 15 na ya kuhuisha 21. Pia maombi ya leseni za uchimbaji mdogo wa madini (PMLs) yalikuwa 4,345 katika Ofisi za Madini za Mikoa na Wilaya kote nchini. Kadhalika, hadi kufikia tarehe 04/07/2017, kulikuwa na jumla ya maombi 240 ya leseni za utafutaji wa madini (PLs). Kati ya maombi hayo, 86 yalishalipiwa ada ya kuandalia leseni (preparation fee) na yaliyobaki hayajalipiwa. Kwa taarifa hii, waombaji wote wa leseni za madini wanatakiwa kukamilisha maombi yao ili yaendane na matakwa ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kama ilivyorekebishwa Mwaka 2017. Hii ni pamoja na:
  • Kulipia ada za kuandalia leseni za madini (PLs, PMLs, MLs na SMLs) kwa maombi yaliyokidhi vigezo vya kupewa leseni;
  • Kuwasilisha Local Content Plan kwa mujibu wa Vifungu vya 102, 103 na 104 vya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kama ilivyorekebishwa na Sheria ya Marekebisho Anuwai ya Sheria zilizoandikwa, Sheria 7 ya Mwaka 2017; kwa waombaji wa leseni za uchimbaji wa kati (MLs) na mkubwa (SMLs) wa madini;
  • Kuwasilisha Corporate Social Responsibility Plan; na tamko la Integrity Pledge kadri ya kifungu cha 105 na 106 kwa mtiririko huo wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kama ilivyorekebishwa Mwaka 2017 kwa waombaji wa leseni za uchimbaji wa kati (MLs) na mkubwa (SMLs) wa madini;
  • Waombaji wote wa leseni za utafutaji wa madini (PLs) kuwasilisha taarifa za technical resources (Mine equipment, technical personnel,…) na Audited Financial Statements;
  • Waombaji wote wa leseni za uchimbaji wa kati (MLs) na mkubwa (SMLs) kuwasilisha Cheti cha Tathmini ya Athari za Mazingira (Environmental Impact AssessmentEIA Certificate), taarifa za Feasibility Studies, technical resources (Mine equipment, technical personnel,…), Audited Financial Statements, uthibitisho wa tathmini ya fidia na kutokuwepo kwa mgogoro/migogoro katika eneo linaloombewa leseni ya uchimbaji wa madini; na
  • Waombaji wote wa leseni za uchimbaji mdogo wa madini (PMLs), baada ya kupata leseni na kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji, wawasilishe Mpango wa Uhifadhi wa Mazingira (Enviromental Protection Plan – EPP );

Nyaraka zote zinazotakiwa, ziidhinishwe na mamlaka zinazohusika na kuwasilishwa kwa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini kupitia Sanduku la Posta 2292, DODOMA.

Imetolewa na:

Prof. Idris Kikula

MWENYEKITI

Mei 11, 2018

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi