Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Spika Dkt. Tulia Ashiriki Mkutano wa Jumuiya ya Madola Ghana
Oct 05, 2023
Spika Dkt. Tulia Ashiriki Mkutano wa Jumuiya ya Madola Ghana
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa kwanza kulia), akifuatilia Mkutano wa 66 wa Kibunge wa Jumuiya ya Madola (CPC) unaoendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Accra nchini Ghana. Kutoka kwa Dkt. Tulia ni Mhe. Abdallah Mwinyi, Mhe. Dkt. Alice Kaijage na Mhe. Dkt. Pius Chaya.
Na Mwandishi Wetu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 5 Oktoba, 2023 ameshiriki Mkutano wa 66 wa Kibunge wa Jumuiya ya Madola (CPC) unaoendelea katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Accra nchini Ghana wenye dhima isemayo “The Commonwealth Charter 10 years on: Values and Principles for Parliaments to Uphold”.

Katika Mkutano huo, Dkt. Tulia ameambatana na baadhi ya Wabunge akiwemo, Mhe. Dkt. Alice Kaijage, Mhe. Abdallah Mwinyi, Mhe. Dkt. Pius Chaya, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama, Mhe. Elibariki Kingu pamoja na Katibu wa Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi