[caption id="attachment_40314" align="aligncenter" width="1000"] Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan akimkabidhi hati ya kiwanja Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Idd wakati wa mara baada ya kufungua Kikao Kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Serikali ya Muungano na Mapinduzi jana jijini Dodoma. Hati hiyo ya kiwanja chenye ukubwa wa Hekari 30 imetolewa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ili waweze kujenga Ofisi zao Makao Makuu ya Nchi jijini Dodoma.[/caption]
Na: Lilian Lundo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameikabidhi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) hati ya kiwanja chenye ukubwa wa heka 30 kilichopo Mji wa Serikali Jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza ujenzi wa ofisi Jijini humo.
Makabidhiano hayo yamefanyika jana wakati wa kikao cha kamati ya pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano kilichofanyika Jijini Dodoma.
[caption id="attachment_40316" align="aligncenter" width="1000"] Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Serikali ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) jana Jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu, Dkt. Hussein Mwinyi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud.[/caption] [caption id="attachment_40318" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Serikali ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) jana Jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_40319" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanziba wakifuatilia kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Serikali ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) jana Jijini Dodoma. (Picha na Frank Shija)[/caption]"Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tunawakaribisha Dodoma, wenzenu tumeanza na nyie tunawategemea kuwepo Dodoma," amesema Mhe. Makamu wa Rais.
Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amesema kiwanja kilichokabidhiwa kwa SMZ kina ukubwa wa sawa na viwanja kumi vilivyogawiwa kwa Wizara, kwani viwanja vya Wizara vinaukubwa wa kati ya heka 3 hadi 5 kwa kila wizara.
Ameendelea kusema, utoaji hati kwa SMZ ni muendelezo wa utekelezaji wa Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhamishia shughuli zake Jijini Dodoma, ambapo tayari wizara zote zimekwisha hamia Jijini humo na mwezi huu zinatarajia kuhamia Mji wa Serikali, uliojengwa eneo la Ihumwa.
Aidha Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameshatoa hati za viwanja kwa Balozi zote zilizopo hapa nchini ili nazo zihamie Jijini humo ambayo ndiyo Makao Makuu ya Nchi.