Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Shindano la Mr. Tanzania kufanyika Desemba
Sep 19, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_14411" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Shirikisho la Wajenga Misuli Tanzania (TBBF) Nemes Chiwalala akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya Mr. Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Desemba 16 leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo na Mkurugenzi wa Pilipili Entertainment Nilesh bhatt, Msemaji wa Pilipili Entertainment Mohamed Ollotu (Mzee Chillo) na Katibu wa TBBF Francis Mapugilo.[/caption]

Na.Paschal Dotto

Chama cha Watunisha Misuli Tanzania (TBBF) kimetangaza kuwa mashindano ya Mr.tanzania, Style, Icon yaani Mr handsome pamoja na Mr photogenic yanatarajiwa kufanyika Desemba 16, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam, leo na Katibu Mkuu wa Chama hicho Bw.Francis Mapungilo alipozungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati ya kuuendeleza mchezo wa kutunisha misuli hapa nchini.

[caption id="attachment_14413" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Mr. Tanzania na Mkurugenzi wa Pilipili Entertainment Nilesh Bhatt akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu mashindano ya Mr. Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam Desemba 16 katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). (Picha na: Frank Shija)[/caption]

Alisema mchezo wa kutunisha misuli ni kama michezo mingine ambayo inaongeza ajira kwa vijana hivyo amewataka vijana kuichangamkia fursa hiyo kwani kwa sasa wameimarisha zaawadi tofauti na hapo awali.

“Mashindano yatakuwa yakioneshwa mubashara kupitia chaneli ya Azam 2 hivyo akawaomba wapenzi na mashabiki wa mchezo huo kuangalia kupitia luninga zao, hii pia itaongeza chachu kwa wanamichezo”, alisema Bw. Mapungilo.

Bw.Mapungilo aliwataka washiriki kuzingatia na kuzielewa kanuni za mchezo huo ili waweze kuchaguliwa kwani miongoni mwa vigezo vitakavyotumika ni kujua taratibu na kanuni za mchezo huo.

Alibainisha kuwa mchakato wa mchujo utaanza Desemba 12, 2017 na huu utakuwa mchujo wa kwanza kutoka kwenye kundi kubwa la washiriki 1000 ambapo katika mchujo huo watatakiwa washiriki 100.

Aidha Bw.Mapungilo alieleza kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kuwa ya haki kwani Majaji  watapewa semina mahususi kuhusu taratibu za mashindano pamoja na Sheria zinazosimamia mchezo huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa (TBBF) Bw.Nemes Chiwalala alisema wanataka kufanya mchezo huo kuwa chanzo cha kipato na ajira kwa vijana kwani mashindano hayo yanafanyika  dunia nzima ambapo mwaka jana mshindi alitoka India.

Aidha Bw. Chiwalala amezungumzia kuwa watakuwa na zawadi nono kwa washindi watatu ambapo mshindi wa kwanza atapata gari aina ya Noah na fedha za kitanzania shilingi 10,000,000 huku mshindi wa pili akichukua 5,000,000 wakati mshindi wa mwisho atapata shilingi 2,500,000.

Kwa upande wa mashindano ya (Mr.handsome na Mr.photogenic na style) Bw. Chiwalala alibainisha kuwa zawadi nono zimeandaliwa kwaajili yao ili kuleta hamasa kwa watanzania waweze kuupenda na kushiriki katika mchezo huo.

Mwigizaji mkongwe nchini Mzee Chillo ambaye ni Msahauri wa kampuni ya ya filamu ya Pilipili, alisema wameamua kuingia mkataba wa miaka mitano na TBBF kwaajili ya kuendeleza mchezo huo nchini Tanzania lengo likiwa kuhakikisha wanatoa washiriki watakaoshiriki katika mashindano ya Dunia yaani Mr.World.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi