Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Shilingi Bilioni 179 za Wadau wa Maendeleo Kupeleka Umeme Vijijini
Sep 19, 2019
Na Msemaji Mkuu

Imeelezwa kuwa, zaidi ya shilingi bilioni 179 zilizotolewa na Wadau wa Maendeleo kama vile nchi za Norway, Sweden, Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU)  na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) zinatarajia kutumika katika mradi wa usambazaji umeme wa ujazilizi ambapo vitongoji  zaidi ya 1103 vinatarajia kufaidika katika mikoaTisa nchini.

Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,  Septemba 18, mwaka huu wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamanenge, Wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu kabda hajawasha umeme.

Mikoa itakayofaidika na mradi huo ni Kilimanjaro, Mbeya, Dodoma, Tanga, Pwani, Shinyanga, Mwanza, Singida na Tabora.

[caption id="attachment_47060" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akiwasha umeme katika kijiji cha Mwamanenge wilayani Maswa mkoa wa Simiyu[/caption]

Alisema, Serikali imeleta umeme wa bei nafuu nchini ili kuleta usawa katika utoaji huduma kwa wananchi wenye vipato tofauti na kwamba wananchi wote waliopitiwa na miondombinu ya umeme watapatiwa nishati hiyo.

“Kwa upande wa Wilaya ya Maswa, matarajio yetu ni kuwa, mapema mwaka 2021 vijiji vyote vya Maswa takriban 125 vitakuwa vimeshaunganishiwa umeme, tumesema hatuchangui nyumba, nyumba zote zitawekewa umeme.” Alisemaa Mgalu

Naye mwananchi wa Kijiji cha Mwamanenge, Rahel Daniel  ambaye nyumba yake iliwashiwa umeme, aliishukuru Serikali kwa kuwajali wananchi wa kipato cha chini kwa kuwawekea bei ya umeme ya shilingi 27,000 ambayo hata wao wameweza kuimudu na alimhakikishia Naibu Waziri kuwa, ataitumia huduma hiyo ya umeme kujiendeleza kiuchumi.

 Naibu Waziri pia aliweka jiwe la msingi katika shule ya sekondari Simiyu iliyopo wilayani Bariadi ambayo  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limejenga baadhi ya vyumba vya madarasa na aliwaasa   wanafunzi hao kusoma kwa bidii na watumie fursa ya umeme kujisomea haswa katika nyakati za usiku.

[caption id="attachment_47063" align="aligncenter" width="750"] 1. Mwananchi wa kijiji cha Mwamanenge Rahel Daniel akitoa shukran kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, baada ya nyumba yake kuunganishwa na huduma ya umeme wa gharama nafuu kupitia mradi wa REA awamu ya tatu.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi