Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yazindua Mwongozo wa Kuomba Mkopo Elimu ya Kati
Oct 04, 2023
Serikali Yazindua Mwongozo wa Kuomba Mkopo Elimu ya Kati
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, akizindua Mwongozo wa Kuomba Mkopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Kati (Diploma) ambao dirisha la uombaji Mkopo litafunguliwa Oktoba 7, 2023, mwongozo huo unapatikana katika tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (www.moe.go.tz), Bodi ya Mkopo ya Elimu ya Juu (www.heslb.go.tz) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (www.nacte.go.tz), maombi yatafanyika kwa siku 15 baada ya kufunguliwa Oktoba 7, 2023.
Na Mawazo Kibamba

Serikali imezindua rasmi Mwongozo wa Kuomba Mkopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Kati watakaodahiliwa  mwaka wa masomo 2023/2024.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 4, 2023 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati akizindua Mwongozo huo katika Ofisi za Bodi ya Mikopo Jijini Dar es Salaam.

“Leo tunazindua Mwongozo huu kwa ajili ya utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Kati katika vyuo vyetu, tunasisitiza wananfunzi wausome vema Mwongozo huo kabla ya kuomba wauone na waelewe nini cha kufanya” amesema Prof. Mkenda.

Waziri Prof. Mkenda amewaeleza Watanzania kuwa serikali inatambua hili limekuwa ni hitaji la muda mrefu na leo limezinduliwa rasmi baada ya kuwa Mhe. Rais Samia kuridhia hilo.

Akifafanua kuhusu mwongozo huo, Prof. Mkenda ameeleza vigezo kwa waombaji wa Mkopo huo kuwa vimewekwa bayana katika tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (www.moe.go.tz), Bodi ya Mikopo ya  Elimu ya Juu (www.heslb.go.tz) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Amali (www.nacte.go.tz)

“Sifa kubwa kwa fani zitakazopewa kipaumbele ni Afya na Sayansi Shirikishi, ualimu wa Fizikia, Hisabati na walimu wa mafunzo ya Amali, Fani ya Usafiri na Usafirishaji hasa mambo ya Anga, Ujenzi wa Reli na Uhandisi pamoja na Nishati” alifafanua Prof. Mkenda.

Aidha, imeelezwa kuwa dirisha la maombi ya mikopo hiyo litafunguliwa rasmi Oktoba 7, na litadumu kwa muda wa siku 15 baada ya kufunguliwa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi