Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali yatoa siku 12 kukamilisha ujenzi wa miundombinu wezeshi mradi wa umeme wa mto rufiji
Sep 29, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_35935" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (mbele) akiwa amefuatana na viongozi mbalimbali wa Serikali kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge, Septemba 28, 2018.[/caption]

Na Veronica Simba – Rufiji

Serikali imeziagiza Taasisi zote zenye jukumu la kujenga miundombinu wezeshi kwa ajili ya Mradi wa Kufua Umeme wa Megawati 2100 kutokana na maporomoko ya Mto Rufiji, kuhakikisha kazi hiyo inakamilika ifikapo Oktoba 10 mwaka huu.

Maelekezo hayo yalitolewa jana, Septemba 28 na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga, katika ziara ya kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu hiyo itakayowezesha kuanza ujenzi wa Mradi husika.

“Tumeridhishwa na kazi zinazofanyika ili kumwezesha Mkandarasi wa Mradi kuanza kazi yake, lakini tunataka kazi zote za ujenzi wa miundombinu wezeshi zikamilike ndani ya siku 12 kuanzia leo,” alisema.

[caption id="attachment_35936" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kulia-mwenye miwani), akikagua zoezi la utandazaji mabomba ya kupitisha umeme chini ya ardhi, katika eneo lenye viwanja vya ndege; akiwa katika ziara kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge, Septemba 28, 2018.[/caption]

Akifafanua zaidi, Waziri Kalemani alisema ni matarajio ya Serikali kwamba kufikia tarehe iliyotolewa, kazi zote zitakuwa zimekabidhiwa serikalini ili kumruhusu Mkandarasi atakayepewa kazi ya kujenga Mradi husika, kuanza rasmi ujenzi.

Kufuatia maelekezo hayo, Waziri Kalemani pia aliwaagiza wakandarasi na mafundi wanaojenga miundombinu wezeshi ya Mradi huo, kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kazi kwa wakati.

Kalemani alimshukuru Naibu Waziri Hasunga kwa kutoa maagizo ya kuhakikisha wanaotekeleza kazi husika hawazuiliwi kufanya kazi usiku kwa kisingizio cha suala la usalama; na kuagiza askari wa wanyamapori waongezwe ili kuimarisha ulinzi utakaowawezesha wahusika kufanya kazi kama walivyoagizwa.

Awali, akielezea kazi za ujenzi wa miundombinu wezeshi ya Mradi, zinazoendelea kutekelezwa; Waziri Kalemani alisema ni pamoja na kuufikisha umeme katika eneo la ujenzi wa Mradi.

[caption id="attachment_35937" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kushoto), akiwasalimia mafundi waliokuwa wakijenga Daraja, akiwa katika ziara kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge, Septemba 28, 2018.[/caption]

“Tayari wameshafikisha umeme kutoka Msamvu, wamekamilisha ujenzi wa vituo viwili vya kupooza umeme vilivyopo Dakawa na Pangawe na wanaendelea kutandaza mabomba yatakayopitisha umeme chini ya ardhi katika maeneo ya viwanja vya ndege viwili. Aidha, kazi ya kuweka nguzo za zege na za miti inaendelea.”

Waziri alitaja kazi nyingine kuwa ni ujenzi wa barabara zote kuelekea kwenye Mradi ikiwemo inayotoka Ubena Zomozi, yenye umbali wa kilomita 178.4 pamoja na ya Kibiti – Lingungu yenye umbali wa kilomita 210. Alisema kazi hii iko katika hatua nzuri.

Nyingine, ni ujenzi wa mitambo ya maji pamoja na matenki makubwa mawili yenye uwezo wa kuhifadhi lita 22,500 hivyo kuweza kuhudumia wafanyakazi takribani 11,000; kazi ambayo imekamilika.

[caption id="attachment_35938" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (mwenye shati la bluu-kulia) akizungumza na mafundi (kushoto), wanaojenga barabara eneo la Rufiji, alipokuwa katika ziara kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge, Septemba 28, 2018.[/caption]

Aidha, Waziri alisema kazi nyingine ni ukarabati wa majengo ya nyumba za wafanyakazi pamoja na ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano kwa njia za simu, ambazo pia zinaendelea na ziko katika hatua nzuri.

Akizungumzia utekelezaji wa Mradi wenyewe wa kuzalisha umeme kutokana na maporomoko ya maji ya Mto Rufiji; Waziri Kalemani alisema utahusisha kazi kuu tatu, ambazo ni pamoja na kujenga Mtambo wa kuzalisha umeme wa megawati 2100.

Vilevile, alisema kuwa kazi nyingine kubwa itahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha umeme kupitia njia mbili; kutoka eneo la Mradi hadi Chalinze, umbali wa kilomita 178 wenye kilovoti 400 na kutoka eneo la Mradi hadi Kibiti kupitia Lungungu, umbali wa kilomita 210 na wenye msongo wa kilovoti 400 pia.

  [caption id="attachment_35939" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (mwenye shati la bluu-kushoto) akitoa maelekezo kwa taasisi mbalimbali za Serikali zinazosimamia ujenzi wa miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge. Waziri alikuwa katika ziara kukagua kazi hiyo Septemba 28, 2018. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga.[/caption]

Aidha, alieleza kazi nyingine kuwa ni ujenzi wa Bwawa lenye eneo la kilomita za mraba 914 lenye uwezo wa kuhifadhi maji kiasi cha mita za ujazo takribani bilioni 35.

Dkt Kalemani aliishukuru na kuipongeza Serikali kwa kutoa fedha za ndani ili kutekeleza Mradi huo mkubwa ambapo alisema mpango wa utekelezaji wake ulipangwa ufanyike tangu miaka ya 1972 mpaka 1980 kwa awamu. “Naipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwakuwa sasa tutaujenga kwa mkupuo.”

Ziara hiyo pia iliwahusisha wabunge wa majimbo ya Rufiji (Omari Mchengelwa), Kibiti (Ally Ungando) na Mafia (Mbaraka Dau), ambao wote walipongeza jitihada za Serikali katika kuhakikisha Mradi huo unatekelezwa.

[caption id="attachment_35940" align="aligncenter" width="750"] Msimamizi wa Miradi ya Ujenzi wa Barabara Mkoa wa Pwani, kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Zuhura Amani (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (wa pili-kulia) kuhusu hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Barabara, wakati wa ziara ya Waziri kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge, Septemba 28, 2018. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Rufiji Omari Mchengelwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga.[/caption] [caption id="attachment_35941" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya mafundi wanaojenga barabara katika eneo la Rufiji, wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), aliposimama kuzungumza nao akiwa katika ziara kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge, Septemba 28, 2018.[/caption] [caption id="attachment_35942" align="aligncenter" width="750"] Taswira ya sehemu ya Mto Rufiji kama ilivyokuwa ikionekana wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge, Septemba 28, 2018.[/caption] [caption id="attachment_35943" align="aligncenter" width="750"] Kazi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya wafanyakazi ikiendelea kama taswira hii ilivyochukuliwa wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge, Septemba 28, 2018.[/caption] [caption id="attachment_35944" align="aligncenter" width="750"] Taswira ya Mtaro uliochimbwa ili kupitisha nyaya za umeme katika eneo la viwanja vya ndege rufiji, kama ilivyonaswa wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge, Septemba 28, 2018.[/caption] [caption id="attachment_35934" align="aligncenter" width="750"] Kazi ya ujenzi wa daraja ikiendelea kama taswira hii ilivyochukuliwa wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge, Septemba 28, 2018.[/caption]

( Picha na  Veronica Simba- Wizara ya Nishati)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi