Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi na Mahusiano, imetangaza nafasi 500 za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye uzoefu katika fani ya udereva wa pikipiki, kwenda kufanya kazi Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Target Tours and Labour Supply Company Limited kutoka nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu ( UAE) imeeleza kuwa ajira hizo zimetolewa na Kampuni ya Velogistic Delivery Service LLC ya UAE.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa waombaji wote wanapaswa kuwa na umri kuanzia miaka 20 hadi 37, elimu ya msingi au sekondari, leseni halali ya udereva wa pikipiki, uzoefu wa angalau miaka miwili katika udereva wa pikipiki, hati ya kusafiria na uwezo wa kuzungumza na kuandika lugha ya Kiingereza.
Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa nafasi hizo zimetengwa kwa waombaji wa kiume pekee huku zoezi la usaili likitarajiwa kuanza Januari 19 hadi 21, 2026 jijini Dar es Salaam, kisha kuendelea katika Mikoa ya Mwanza kuanzia Januari 22 hadi 24, Tanga kuanzia Januari 26 hadi 28, 2026.
Serikali inatoa wito kwa vijana wenye sifa kote nchini kuchangamkia fursa hiyo kama sehemu ya mkakati wa kupanua ajira kwa Watanzania kupitia ushirikiano wa kikanda na kimataifa.
Aidha, waombaji wote wanatakiwa kutuma wasifu (CV) zao kupitia anuani ya info@targettours.co.tz au kupiga simu
namba +255784989905,
+255766712222,