Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yataifisha Ng’ombe 6,648 Misenyi Kagera
Nov 02, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_21555" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Misenyi mara baada ya zoezi la kutaifisha ng'ombe.[/caption]  

Na. MWANDISHI MAALUM MISENYI.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina Ameagiza kukamilishwa  kwa taratibu za Uhamiaji na Mahakama kupitia mwanasheria mkuu wa Serikali, wa Wilaya ya Misenyi Pamoja na Uhamiaji, ili kuweza kupigwa mnada kwa idadi ya ng’ombe 6648 walioingia nchini kinyemela toka nchi jirani ya Uganda na kukamatwa.

Waziri mpina alisema uvamizi wa kundi kubwa kama hilo la wanyama linaweza kusabisha madhara makubwa katika mazingira kama vile mmomonyoko wa ardhi, kuharibifu wa vyanzo vya maji, kumaliza malisho ya mifugo iliyoko nchini, kusababisha migogogoro ya mara kwa mara kwa wakulima na wafugaji na hata kuleta maambukizi ya magonjwa ya wanyama.

“Sisi kama Serikali hatuwezi kuruhusu hali hii iendelee na mimi kama Waziri Mwenye dhamana nina jukumu la kuhakikisha tunalinda rasimali hii ya malisho” Alisema Mpina.

[caption id="attachment_21556" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya ng'ombe 6638 waliotaifishwa na Serikali baada ya kuingia nchini kinyemela kutoka nchi jirani ya Uganda ng'ombe hao wanasubiri maamuzi ya Mahakama kwa ajili ya Kupigwa mnada.[/caption]  

Waziri Mpina alisema suala hili haliingiliani na Ushirika wa Afrika Mashariki kwani Ushirika huo upo kisheria hivyo wavamizi wanaoingiza mifugo kinyemela nchini toka nchi jirani ni wahalifu kama wahalifu wengine.

“Kwa hiyo naangiza ng’ombe hawa 6,648 waliokamatwa hatua ziendelee na ambao hawajakamatwa wakamatwe na wataifishwe na Serikali.”Alisisitiza Waziri Mpina.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Kanali Denis Mwila alisema kuwa zoezi la kutathmini ng’ombe katika Wilaya yake bado linaendelea na taratibu za kisheria zinafuatwa.

Alipokuwa Mkoani Kagera alitembelea mabwawa ya mradi wa  samaki yaliyopo Wilayani Muleba katika kijiji cha Luhanga na kusema Serikali ina nia ya kukomesha kabisa uvuvi haramu ikiwa ni pamoja na kuwasaka wavuvi haramu kule waliko na  kuwa na nyenzo.

Aidha, akiwa Bukoba Mjini Mpina alitembelea kiwanda cha kuchakata samaki cha Suprime Fish Ltd na kuagiza wamiliki wa viwanda vya samaki nchini kuhakikisha wanachukua hatua za haraka kufufua viwanda hivyo na kuongeza uzalishaji.

   

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi