Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yasimika Taa za Kuongozea Magari Jijini Tanga
Sep 05, 2017
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_11995" align="aligncenter" width="750"] Mafundi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakifunga mabomba ya chuma kwa ajili ya kusimika mfumo wa taa za kuongozea magari katika makutano ya barabara za Taifa na Pangani jijini Tanga.[/caption]

Na Theresia Mwami – TEMESA

Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) inatekeleza miradi miwili ya taa za kuongozea magari (traffic lights) Jijini Tanga katika makutano ya barabara za Taifa na Pangani, pamoja na makutano ya barabara za Swahili, Uhuru na ile inayoelekea hospitali ya Bombo.Mji wa Tanga haujawahi kuwa na taa za kuongozea magari.

Akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Tanga Meneja wa Kikosi cha Umeme TEMESA Mhandisi Pongeza Semakuwa alisema miradi hii miwili ya taa za barabarani Jijini Tanga inahusisha taa za kuongozea magari pamoja na zile za kuongoza waenda kwa miguu kuvuka katika makutano ya barabara.

Alisema taa hizo za kisasa zitakuwa zikitumia umeme jua, nishati ambayo itaziwezesha kufanya kazi muda wote hata pale umeme wa TANESCO unapokuwa na hitilafu au umekatika.

[caption id="attachment_11996" align="aligncenter" width="750"] Mafundi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakiunganisha nyaya kwenye “Panel za Solar” zitakazotumika katika mfumo wa taa za kuongozea magari na abiria (traffic lights) katika makutano ya barabara za Taifa na Pangani Jijini Tanga.[/caption]

Nae Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe. Alhaj Mussa Mbaruku  alipopita kwenye eneo la mradi “Taifa/Ring Junction” kujionea utekelezaji  wa mradi wa Serikali, alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutapunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikitokea kwenye makutano ya barabara, pia  kuufanya Mji wa Tanga kuwa wa kisasa zaidi.

Kwa upande wake Meneja wa TEMESA Tanga Mhandisi Margareth Gina alisema kuwa miradi hiyo ya usimikaji wa taa za kuongozea magari na waenda kwa miguu Jijini Tanga imeiingizia TEMESA jumla ya shilingi milioni 434 fedha za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitakazolipwa kwa TEMESA kupitia ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Tanga.

[caption id="attachment_11997" align="aligncenter" width="750"] Mafundi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakifunga taa za kuongozea magari (traffic lights) katika makutano ya barabara za Taifa na Pangani jijini Tanga[/caption] [caption id="attachment_11998" align="aligncenter" width="750"] Mbunge wa Tanga Mjini Mhe. Alhaj Mussa Mbaruku akiongea na watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) alipofika katika eneo la mradi wa kusimika taa za barabarani katika makutano ya barabara za Taifa na Pangani jijini Tanga . kutoka kushoto ni Mhandisi Zuhura Semboja, Mhandisi Pongeza Semakuwa pamoja na Mhandisi Margaret Gina.Picha zote na Theresia Mwami - TEMESA[/caption]    

Mhandisi Gina alisema miradi hiyo  miwili inatarajiwa kukamilika mapema mwezi huu na kuwataka wakazi wa Jiji la Tanga kuilinda miundombinu hiyo kwani imegharimu fedha nyingi za serikali.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi