Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yaridhishwa na Maendeleo ya Mradi wa Maji Chalinze
Jul 19, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_7044" align="alignnone" width="750"] Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akioneshwa ramani ya mradi huo na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wake wakati alipofanya ziara kukagua mradi huo wa ukarabati na upanuzi wa mtambo wa maji Chalinze na na ujenzi wa mfumo wa kusafirishia maji pamoja na matenki yakuhifadhia maji.[/caption]

Na. Frank Mvungi-Maelezo

Serikali imesema kuwa inaridhishwa na hali ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa mtambo wa maji Chalinze na ujenzi wa mfumo wa kusafirishia na kusambaza maji pamoja na matenki ya kuhifadhi maji utakaozalisha zaidi lita milioni tisa utakapokamilika.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua mradi huo utakaonufaisha wakazi zaidi ya laki tatu wa Jimbo la Chalinze na Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga, Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Ezekiel Kamwele amesema dhamira ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuona wananchi wanapata huduma ya maji kwa wakati kupitia maradi huo unaotarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu.

“Mradi wa Lindi umekamilika na hapa lazima tuchukue hatua kama Lindi ili kutatua changamoto zinazoweza kukwamisha kukamilika kwa mradi kwa wakati  na kwa kuwa wametupa mpango kazi wao tunaamini kazi itakamilika kwa wakati na nitafuatilia kila hatua “ Alisisitiza Mhandisi Kamwele.

[caption id="attachment_7045" align="alignnone" width="1000"] Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akisisitiza jambo wakati wa ziara yake  ya kukagua hatua iliyofikiwa katika mradi wa ukarabati  na upanuzi wa mtambo wa maji chalinze na ujenzi wa mfumo wa kusafirishia maji pamoja na matenki yakuhifadhia maji. Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Chalinze (CHALIWASA), Mhandisi Christer Mchomba na kushoto ni Msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya WAPCO inayotekeleza mradi huo.[/caption]

Akifafanua Mhandisi Kamwele amesema kuwa katika kila eneo la mradi alilokagua ikiwemo ulazaji wa mabomba, ujenzi wa matenki ya kusambazia maji ameridhishwa na kasi ya utendaji na kuipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASA) kwa usimamizi mzuri katika utekelezaji wa miradi ya maji wanayokabidhiwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Chalinze (CHALIWASA) Mhandisi Christer Mchomba amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kukuza shughuli za kiuchumi zikiwemo za viwanda kwa kuwa tayari wamepokea maombi ya Viwanda kadhaa kuunganishwa katika mtandao wa maji,viwanda hivyo ni Kiwanda cha shurubati (juisi), Kiwanda cha kutibu mbao, pamoja na Kiwanda cha kuzalisha vigae.

[caption id="attachment_7048" align="aligncenter" width="900"] Mafundi wakiendelea na Kazi ya ujenzi wa matanki ya kuhifadhi na kusambaza maji katika Jimbo la Chalinze.[/caption] Aliongeza kuwa mradi huo pia utasidia kuinua shughuli za Kilimo na ufugaji hali itakayosaidia kukua kwa sekta ya Viwanda hali itakayochochea kukua kwa uchumi.

“Awamu ya Tatu ya mradi huu inagharimu bilioni 84 hadi kukamilika kwake na huu ni mradi mkubwa utakaowanufaisha wananchi wengi” Alisisitiza Mhandisi Mchomba.

Katika kutekeleza mradi huo ulazaji wa mabomba ya kusafirishia maji umefikia km 96.8 kati ya km 115 na ujenzi wa ofisi umefikia asilimia 82.

[caption id="attachment_7052" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya mabomba yakiwa katika moja ya maeneo unakotekelezwa mradi huo.[/caption]

Kwa upande wake Mwenyekiti mstaafu wa Kijiji cha Rupungwi Chalinze ambacho ni sehemu ya vijiji vinavyonufaika na mradi huo amesema wananchi wanapongeza Serikali kwa kuwaletea mradi huo utakaoinua shughuli za kiuchumi.

Mradi huu unatekelezwa kupitia mkopo kutoka India na mkataba wa ujenzi ulisainiwa tarehe 18 Mei, 2015 kati ya DAWASA na Kampuni ya Overseas Infrastracture Pvt Ltd ikishirikiana na PIL zote za India

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi