Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yakabidhi Pikipiki 32 kwa Maafisa Elimu Kata Wilayani Moshi
Sep 20, 2018
Na Msemaji Mkuu

 

Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi pikipiki 32 kwa Maafisa Elimu kata waliopo katika wilaya ya Moshi.
Baadhi ya Mafisa Elimu Kata katika Halmashauri ya wilaya ya Moshi wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,katika hafla fupi ya kukabidhi pikipiki kwa ajili ya kusaidia katika Sekta ya Elimu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi ,Michael Kilawila akiungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Tatu Kikwete akizungumza katika hafla hiyo.
Kaimu Afisa Elimu Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Abdalah Komesha akisoma taarifa kuhusu makabidhiano ya pikipiki hizo ambazo zimetolewa kwa Maafisa Elimu kata hao.
Mwakilishi wa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Brabarani mkoa wa Kilimanjaro,Meja Hilda Mlay akitoa elimu ya usalama barabarani kwa Maafisa Elimu kata ambao wamekabidhiwa pikipiki kwa ajili ya kurahisisha kazi zao.
Mkaguzi wa Magari wa Polisi ,Francis Arthur akitoa elimu namna ya kutumia pikipiki kwa watendaji hao.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akikabidhi funguo ya  pikipiki kwa mmoja wa Maafisa Elimu kata wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya pikipiki hizo ambazo zitasaidia katika kukuza Elimu kupitia mradi wa KKK.kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila na mwisho ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Tatu Kikwete.
Maafisa Elimu kata wakiwa wamevalia kofia ngumu tayari kuanza safari mara baada ya kukabidhiwa pikipiki kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi wao.
Sehemu ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa Maafisa Elimu kata ,katika Halmashauri ya wilaya ya Moshi.
 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi