Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yajivunia Kutokomeza Mbung'o Miaka 60 ya Muungano
Apr 16, 2024
Serikali Yajivunia Kutokomeza Mbung'o Miaka 60 ya Muungano
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Hamisi Ulega akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Sekta ya Mifugo na Uvuvi katika kipindi cha miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Aprili 16, 2024 jijini Dodoma.
Na Ahmed Sagaff - Maelezo

Serikali imesema imefanikiwa kuwatokomeza wadudu aina ya mbung'o wakati Watanzania wakiadhimisha miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akieleza mafanikio hayo ya muungano, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema mbung'o husababisha ugonjwa wa Malale kwa binadamu na ugonjwa wa Nagana kwa mifugo.

"Serikali imeweza kutokomeza mbung'o katika kisiwa cha Unguja kwa kutumia mbung'o hasi ambao walizalishwa katika maabara ya Kituo cha Utafiti wa Mbung'o na Ndorobo kilochopo Tanga," amearifu Waziri Ulega.

Waandishi wa Habari mkoani Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Hamisi Ulega wakati akizungumza nao kuhusu mafanikio ya Sekta ya Mifugo na Uvuvi katika kipindi cha miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Aprili 16, 2024 jijini humo.

Pamoja na hilo, Mhe. Ulega amefahamisha kuwa sekta ya uvuvi imechangia asilimia 6.7 kwenye pato la Taifa kwa mwaka 2022 ikiwa Tanzania ni nchi ya pili katika orodha ya nchi zenye idadi nyingi za mifugo barani Afrika.

"Udumu muungano wetu na yadumu maono ya waasisi wetu kwa kuwa muungano wetu ni tunu yetu na sisi lazima tujifaharishe na yaliyoasisiwa na viongozi wetu. Yeyote atakayeonekana yuko kinyume na muungano wetu, ni adui yetu," ameeleza Waziri Ulega.

Tanganyika na Zanzibar ziliungana Aprili 26, 1964 kwa kuchanganya udongo wa nchi hizo mbili zilizounda Taifa moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi