Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yaipongeza MUWSA kwa Kuwa Mamlaka Bora ya Maji Mashariki na Kusini mwa Afrika
Dec 20, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_39119" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof.Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuipongeza Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Mjini Moshi kuwa Mamlaka bora ya maji Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika leo Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Bibi.Joyce Msiru.[/caption]

Serikali imeipongeza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini MoshI (MUWSA) kwa kuwa mshindi wa jumla kati ya Mamlaka nane zilizoshindanishwa na Jumuiya ya Taasisi za Udhibiti wa Sekta ya Maji zilizopo katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAWAS).

Pongezi hizo zimetolewa leo  Jijini Dodoma na Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo  wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuipongeza Mamlaka hiyo kwa kufanya vizuri  katika shindano hilo.

[caption id="attachment_39120" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof.Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuipongeza Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Mjini Moshi kuwa Mamlaka bora ya maji Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika leo Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Bibi.Joyce Msiru.[/caption]

Prof. Mkumbo amesema kuwa katika mchakato huo, Taasisi ya ESAWAS ilishindanisha Mamlaka moja bora kutoka kila nchi wanachama na kupata mshindi wa jumla kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ambapo kwa Tanzania mamlaka bora katika kutoa huduma ya maji mwaka 2016/17 ilikuwa MUWSA.

“Katika kikao cha mkutano mkuu (AGM) kilichofanyika Novemba 2018, Taasisi hii iliitangaza rasmi MUWSA kuwa mshindi wa jumla kwa kupata 79.9% ikifuatiwa na WASAC ya Rwanda kwa 77.4% na Nyeri ya Kenya ikifuatia kwa 70.8% hivyo wizara inaipongeza MUWSA kwa kazi nzuri katika kutoa huduma ya maji na tunaamini itakuwa kichocheo kwa mamlaka zingine za maji kuongeza juhudi,” alisema Prof. Mkumbo.

Prof. Mkumbo amevitaja vigezo vitatu vilivyotumika kushindanisha mamlaka hizo vikiwemo vya Ubora wa Huduma, Ufanisi wa Kiuchumi, na Uendelevu wa Mtoa Huduma ambapo MUWSA imekuwa mshindi wa kwanza katika eneo la Uendelevu wa Huduma kwa kupata 94.6%.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MUWSA, Bi. Joyce Msiru amesema kuwa mafanikio ya ushindi huo yametokana na ushirikishwaji mkubwa wa wadau na Bodi ya mamlaka hiyo pia kwa 100% Manispaa ya Moshi ina maji yenye ubora wa hali ya juu katika kila eneo.

Upatikanaji wa maji safi na yenye ubora wa hali ya juu katika maeneo yote ya Manispaa ya Moshi ndio unaofanya hata Manispaa hiyo kuwa Jiji safi kuliko majiji mengjne nchini”, alisema Bi. Joyce.

Jumuiya ya Taasisi za Udhibiti wa Sekta za Maji zilizopo katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika inaundwa na nchi za Kenya, Msumbiji, Rwanda, Tanzania, Lesotho, Zambia, Burundi na Zanzibar, hii ni mara ya nne tangu mashindano hayo yaanze kufanyika.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi