Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Yaimarisha Maabara Kupima Washukiwa wa Corona
Apr 06, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_52050" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati alipohitimisha hoja kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa Mwaka 2020/2021, Bungeni jijini Dodoma, Aprili 6, 2020.[/caption]

Jonas Kamaleki, Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imeimarisha maabara nchini kwa ajili ya kupima washukiwa wa ugonjwa ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (COVID-19) unaosababishwa na virusi vya Corona.

Amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo kwani upimaji huo utafanyika kote nchini badala ya kutegemea sehemu moja. Waziri Mkuu ametaja maabara hizo kuwa ziko Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Mbeya, Mwanza, Morogoro, Kigoma, Pwani  na Dodoma.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Bungeni, jijini Dodoma wakati alipohitimisha hoja  kuhusu  Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa Mwaka 2020/2021.

Aidha, Waziri Mkuu amesema hadi leo mchana hapa nchini kuna wagonjwa 24 waliothibitika kuwa na ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (COVID-19) ambapo watatu kati yao wamepona na kuruhusiwa kutoka hospitali, mmoja amefariki dunia na wagonjwa 20 wanaendelea vema na matibabu.

“Serikali imeendelea kuwafuatilia watu 685 waliokutana na wagonjwa hao ambapo watu 289 amemaliza siku 14 za kufuatiliwa na vipimo vyao vimethibitisha kuwa hawana maambukizi ya virusi vya Corona. Watu wengine 396 waliobaki wanaendelea kufuatiliwa ili kujiridhisha iwapo hawana maambukizi ya virusi hivyo,” amsema Waziri Mkuu Majaliwa.

Amesema hatua zinazochukuliwa katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona ni pamoja na kufanya ukaguzi (screening) kwa wageni wote wanaoingia nchini kutoka nje pamoja na kuwaweka katika uangalizi kwa siku 14.

“Ndege zetu tumezuia kufanya safari za nje, tumezuia wafanyakazi kwenda nje ya nchi,tumeimarisha mipaka sambamba na kuhakikisha wasafiri wote wanaoingia nchini wanalazimika kuwekwa chini ya uangalizi wa lazima kwa siku 14 kwa lengo la kudhibiti mienendo ya wasafiri chini ya ulinzi wa masaa 24,” amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu amesema kutokana na umuhimu wa kuwatenga watu wanaofuatiliwa, Serikali imeagiza mikoa yote nchini itenge maeneo maalumu kwa ajili ya uangalizi na kujiridhisha iwapo hawana maambukizi.

Ameongeza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kudhibiti kuenea zaidi kwa maambukizi ya virusi vya Corona. Kati ya hao, wengi ni wale waliotoka nje ya nchi. Maeneo hayo yametengwa kwa nia njema na yako kwa viwango tofauti kulingana na uwezo wa kifedha wa wahusika. Yako mabweni, ziko nyumba, na vyote vimewekwa kwa kuzingatia gharama mtu anayoweza kumudu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi